KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, June 19, 2012

Mapingamizi Yanga kusikilizwa kesho.

Jaji Mkwawa akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga(picha kwa msaada Bin Zubeir)
Wagombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mdogo wa klabu ya Yanga waliowekewa pingamizi wakiongozwa na Yusufu Manji na Sarah Ramadhani wanaowania nafasi ya Mwenyekiti , , Yono Kevella, Clement Sanga na Ally Mayay wanao wania nafasi ya makamu mwenyekiti wametakiwa kukutana uso kwa uso na wanachama wa clabu hiyo walioweka pingamizi katika makao makuu ya klabu hiyo ili kusikiliza mapinfgamizi yao.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu ya Yanga Jaji John Mkwawa amewaambia waandishi wa habari hii leo kuwa wagombea hao wanapaswa kufika katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo katika makutano ya mitaa ya  Twiga na Jangwani kesho saa 4:00 asubuhi kusikiliza na kukabiliana na mapingamizi yao.

No comments:

Post a Comment