Mashabiki kadhaa wa soka wamejeruhiwa kufuatia uzio kuvunjia wakati wakishangilia kwa mtindo maarufu barani Amerika ya kusini unaotambuliaka kama 'avalanche' katika mchezo wa michuano ya Libertadores nchini Brazil.
Aina hiyo ya ushangilia hufanyika katika nchi zote zilizo barani humo ambapo mashabiki huwa wanarukaruka kutoka ngazi moja ya jukwaa kwenda mbele huku wakiimba wakinogesha na kuleta mvuto wa mtindo huo wa ushangliaji wa 'Avalanche'.
Uzio ulivinjika baada ya Elano kuifungia Gremio goli kunako dakika ya 16.
Kushangilia kunahitaji mashabiki kuruka ruka kwenda mbele ya jukwaa kupata ladha ya Avalanche.
Mashabiki kadhaa waliangukia katika mtaro unaogawanya sehemu ya kuchezea na jukwaa.
Mchezo huo ulikuwa unazikutanisha Gremio dhidi ya Brazil dhidi ya Liga de Quito ya Equador katika dimba la Porto Alegre ambapo mashabiki walikuwa wakishangilia bao la dakika ya 16 lilifungwa na Elano.
Vyombo vya habari nchini Brazil vimearifu kuwa watu 8 wamejeruhiwa katika tukio hilo.
Tukio hilo limetokea katika uwanja uliokamilika wa Arena Gremio, ambao si miongoni mwa viwanja vitakavyotumika katika michuano ya mwaka huu ya 'Confederations Cup' na michuano ijayo ya kombe la dunia nchini Brazil.
Arena Gremio ulitumika December 8 kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa baina ya Gremio dhidi ya Hamburg.
Pia kulifanyika mchezo mwigine December 19 pale ambapo mshambuliaji mkongwe wa Brazil alipokuwa akicheza mchezo wa hisani dhidi ya timu iliyoundwa na mkongwe mwenzake kutoka nchini Ufaransa Zinedine Zidane.
No comments:
Post a Comment