KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, January 31, 2013

ASHLEY COLE KUKAMILISHA MCHEZO WA 100 DHIDI YA BRAZIL. ROY HODGSON ATANGAZA KIKOSI.

Ashley Cole at Reading
Kocha wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson ametangaza kikosi cha timu yake kitakacho ikabili Brazi jumatano ijayo katika dimba la Wembley.
Katika kikosi hicho mlinzi wa pembeni Ashley Cole naye amejumuishwa ili aweze kukamilisha mchezo wa 100 kuitumikia timu ya taifa ya England kupitia mchezo huo dhidi ya Brazil licha ya nafasi finyu ya kupata nafasi katika kikosi cha kwanza mbele ya Leighton Baines.

Mchezo huo ni maalum kwa ajili ya kuadhimisha miaka 150 ya chama cha soka nchini England FA.

Roy Hodgson amemjumuisha tena Chris Smalling ndani ya kikosi kama ilivyo kwa Leon Osman ambaye atakuwepo katika mchezo huyo dhidi ya Brazil.
Hodgson amewataja wachezaji 24 tayari kuikabili Brazil ambao ni waandaaji wa michuano ijayo ya kombe la dunia.

Wakati John Ruddy na Fraser Forster wakiwa majeruhi Hodgson amemjumuisha Joe Hart na mlinda mlango kinda Jack Butland, ambaye yuko katika tetesi kubwa za uhamisho katika kipindi hiki.
Mlinzi wa Chelsea Cole amejumuishwa na hii ni nafasi yake ya kuwa ni mchezaji wa 7 wa England kufikisha jumla ya michezo 100 ya kuitumikia timu ya taifa.
Facing off: England last played Brazil in Doha in 2009
Wachezaji waliokuwepo katika kikosi kilichocheza na Brazil kwa mara ya mwisho mwaka 2009 mjini Doha Steven Gerrard, Frank Lampard na Wayne Rooney wote wameitwa ikiwa ni pamoja na mshambuliaji wa Tottenham Jermain Defoe, ambaye amekuwa na matatizo ya nyonga.
Pengine chaguo la kushangaza linaweza kuwa ni kuingizwa kikosini kwa mchezaji Gareth Barry ambaye amekuwa katika kiwango safi katika kikosi cha Manchester City lakini amekuwa akikosekana katika kikosi cha England tangu apatwe na majeraha katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Norway na hakuitwa katika michuano ya Euro 2012.
Hodgson amemuacha kinda wa Manchester United Phil Jones ambaye amekuwa akifanya vizuri katika kikosi cha England cha Under 21.
Flair player: Ronaldinho is back in the Brazil squad for the game at Wembley
Ronaldinho amerejeshwa katika kikosi cha Brazil dhidi ya England utakaopigwa jumatano katika dimba la Wembley.
Hurdle to jump: Wayne Rooney is challenged by Thiago in Doha
Wayne Rooney.
Striking: Theo Walcott is hoping to continue his club form at international level
Theo Walcott anatarajiwa kuwa katika kiwango kilekile kama ilivyo katika klabu yake ya Arsenal.
Keeping them out: QPR goalkeeper Julio Cesar is back in the Brazil squad as reward for his fine form
Mlinda mlango wa QPR Julio Cesar amerejeshwa katika kikosi cha Brazil baada ya kuwa vizuri katika kiwango.

 KIKOSI KAMILI CHA ENGLAND DHIDI YA BRAZIL
Goalkeepers: Jack Butland (Birmingham), Joe Hart (Man City).
Defenders: Leighton Baines (Everton), Gary Cahill (Chelsea), Ashley Cole (Chelsea), Phil Jagielka (Everton), Glen Johnson (Liverpool), Joleon Lescott (Man City), Chris Smalling (Man Utd), Kyle Walker (Spurs).
Midfielders: Michael Carrick (Man Utd), Tom Cleverley (Man Utd), Steven Gerrard (Liverpool), Frank Lampard (Chelsea), Aaron Lennon (Spurs), James Milner (Man City), Leon Osman (Everton), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Theo Walcott (Arsenal), Jack Wilshere (Arsenal).
Forwards: Jermain Defoe (Spurs), Wayne Rooney (Man Utd), Daniel Sturridge (Liverpool), Daniel Welbeck (Man Utd)

No comments:

Post a Comment