Beckham akiwasili zahanati ya Pitie-Salpetriere kwa vipimo vya afya kabla ya kukamilisha taratibu za uhamisho wa kujiunga na PSG.
|
David Beckham anatarajiwa kujiunga na Paris Saint-Germain.
Sambamba naye ni nyota wa klabu ya Roma Daniele De Rossi na nyota mwingine wa Napolo Marek Hamsik.
Kiungo huyo alikuwa ni mmoja wa wachezaji wenye majina makubwa waliokuwa katika mapango wa Carlo Ancelotti na nahodha huyo wa zamani wa England anatarajiwa kutambulishwa baadaye hii leo jijini Paris.
Beckham amekuwa ni mchezaji huru tangu amalize mkataba wake na LA Galaxy mwezi November na alikuwa akifanya mazoezi ya kujiweka fiti na Arsenal.
Kiungo huyo pia alikuwa akihusishwa na safari ya kujiunga na klabu hiyo yenye maskani yake jijini Paris Ufaransa mwaka jana kabla ya kumalizia mwaka mmoja kati ligi ya Marekani ya MLS.
Ancelotti ambaye aliwahi kuwa meneja wa Beckham wakati huo akiifundisha AC Milan, hapo kabla alinukuliwa akikanusha taarifa za kwamba alikuwa akimuwania kiungo huyo.
Alinukuliwa mwezi uliopita akisema.
'Najua kuwa ameondoka Los Angeles Galaxy, lakini hatumuhitaji'.
Beckham akianza safari ya kuelekea Paris kutoka London asubuhi ya leo.
Kesho PSG itakuwa uwanjani dhidi ya dhidi ya Toulouse hapo kesho ambao ni mchezo wa ligi kuu ya nchini Ufaransa League 1.
PSG iko kileleni katika msimamo wa ligi na inadhaniwa kuwa uzoefu wa kutwaa mataji wa Beckham huenda ukawa ni chachu ya PSG kuipiga kumbo Lyon na kutwaa taji la ligi kuu ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment