Mama Fauziat Abood akiongea na waandhishi wa habari katika ofisi za shirikisho la soka nchini kuelezea juu ya kampeni ya kutokomeza malaria kupitia mpira wa miguu. |
Taasisi
inayojishughulisha na kampeni ya kuzuia, kupambana na kutokomeza malaria nchini
ya taasisi ya Johns Hopkins imesema kuwa inaendelea na shughuli zake kwa kushirikiana na shirikisho la soka nchini Tanzania TFF kupitia timu ya taifa, kwa lengo la kufanikisha kampeni yao.
Akiongea na waandhishi wa habari mwakilishi wa taasisi hiyo nchini ambaye pia ni mtangazaji mkongwe Fauziat Abood amesema taasisi yake inafarijika kufanya kazi na TFF kwa lengo la kutokomeza malaria chini ambapo wamekuwa wakiweka matangazo ya kampeni hiyo bure.

Amesema kwa kutumia kauli mbiu ya tuungane kutokomeza malaria ambayo ilizindiliwa kwa kengo moja na ambalo limetokana na malengo ya milenia wataendelea kutoa ujumbe kupitia mpira wa miguu kama imbavyo imekuwa ikifanyika sehemu mbalimbali barani Afrika.
Amesema mradi huo ulizinduliwa rasmi mwaka 2010 wakati huo chini waziri wa afya akiwa ni mheshimiwa David Mwakyusa ambapo wamekuwa wakiwatumia wachezaji wa soka na kuweka mabango ya kampeni hiyo viwanjani.
Ametolea mfano michuano ya kombe la Kagame iliyopita taasisi yao ilitumia fursa hiyo kufanya kampeni yake viwanjani lakini pia kutumia baadhi ya wachezaji kuhakikisha ujumbe unafika katika jamii.
Kwasasa kampeni hiyo inaendelea kufanyika nchini Afrika Kusini ambako mashindano ya mataifa ya Afrika AFCON yanaendelea.
Katika kuunga mkono mashindano ya afrika kusini wamechapisha gazeti linalo iitwa GOAL ambalo ndani yake kuna ratiba ya michezo ya mataifa ya Afrika na ujumbe ukitolewa na baadhi ya wachezaji wakubwa ambao wametoa ujumbe wa kupiga vita malaria.

Taasisi ya Johns
Hopkins chini ya mradi huo wa tuungane kutokomeza Malaria (United Against
Malaria (UAM)) ilizindua toleo la tatu la jarida lake rasmi kwa ajili ya
fainali za mataifa ya Afrika linalo tambulika kama “Afcon 2013 Goal Malaria Magazine” ikiwa ni
sehemu ya kampeni ya kupiga vita malaria barani Afrika.
Jarida hilo
lenye kurasa 8 linazungumzia juu ya kuzuia, kujihadhari na kuondoa malaria
kupitia mpira wa miguu ambapo wachezaji kadhaa wakubwa kutoka barani Afrika
wametumika katika kutoa ujumbe juu ya kampeni ya kupambana na malaria wakiwemo Didier
Drogba, Christopher Katongo, Samuel Etoo Fils, Stephen Pienar na Alhaji Issah
Hayatou Rais wa shirikihso la soka barani Afrika (CAF).
No comments:
Post a Comment