Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya TFF Deogratius Lyato. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAAMUZI KUHUSU PINGAMIZI DHIDI YA WAOMBAJI UONGOZI
WA TFF NA TPL BOARD
31 JANUARI 2013
Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(4) katika
kikao chake kilichofanyika tarehe 30 Januari 2013, ilijadili pingamizi
zilizowekwa dhidi waombaji uongozi wa TFF na TPL Board na kutoa maamuzi
kama ifuatavyo:
1. Waombaji uongozi wa TPL Board
(a) Pingamizi dhidi ya Ndg. Said Muhammed Abeid anayeomba kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili pingamizi iliyowasilishwa na Ndg. Frank M. Mchaki dhidi ya Ndg. Said Muhammed, aliyeoomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF kumwondoa mwombaji uongozi kugombea nafasi aliyoomba, kwamba Ndg. Said Muhammed:
(i) Si Mwenyekiti wa Klabu ya Azam na hivyo hana sifa za kugombea uongozi wa TPL Board.
(ii) Si mkweli katika maelezo aliyoyatoa kwenye fomu yake ya maombi ya uongozi.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF ilipitia maelezo ya Mweka pingamizi na ilijiridhisha
kuwa pingamizi iliyowasilishwa mbele yake na Ndg. Mchaki haikukidhi
matakwa Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kuwa
haikuambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya
pingamizi. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeitupa pingamizi hiyo.
(b) Pingamizi dhidi ya Ndg. Yusufali Manji anayeomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili pingamizi zilizowasilishwa na Ndg. Daniel T. Kamna na Ndg. Juma Ally Magoma walioomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF kumwondoa mwombaji uongozi kugombea nafasi aliyoomba, kwamba Ndg. Yusufali Manji :
(i) Hana uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5) wa uendeshaji wa mpira wa miguu.
(ii) Hana
sifa ya kuwa ama mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi au kushiriki
katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu katika ngazi ya Mkoa au Ligi daraja
la kwanza.
(iii) Hana elimu ya kidato cha nne
(iv) Ameshindwa kusimamia katiba ya Young Africans Sports Club Ibara ya 10(6), 18(1)b, 27 (2) na (5).
Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilipitia pingamizi hizo na ilijiridhisha kuwa pingamizi zilizowasilishwa mbele yake na Ndg. Daniel T. Kamna na Ndg. Juma Ally Magoma
hazikukidhi matakwa Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kuwa
hazikuambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya
pingamizi. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imezitupa pingamizi hizo.
(c) Pingamizi dhidi ya Ndg. Hamad Yahya Juma anayeomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili pingamizi iliyowasilishwa na Ndg. Frank M. Mchaki dhidi ya Ndg. Hamad Yahya Juma, kwamba Ndg. Hamad Yahya Juma:
(i) Si Mwenyekiti wa Klabu ya Mtibwa na hivyo hana sifa za kugombea uongozi wa TPL Board.
(ii) Si mkweli na mwadilifu na amekuwa akijipachika cheo cha mwenyekiti wa klabu.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeitupa pingamizi ya Ndg. Frank M. Mchaki kwa kuwa pingamizi iliyowasilishwa mbele yake haikukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kutoambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi.
2. Waombaji uongozi wa TFF
(a) Pingamizi dhidi ya Ndg. Athumani K. Kambi
anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF
kupitia Kanda ya 9 (Mtwara na Lindi): Ndg. Kambi aliwekewa pingamizi
kwamba amefanya Kampeni kabla ya muda uliopangwa.
Kamati imeitupa pingamizi ya Ndg.
Jeremiah John Wambura kwa kuwa mweka pingamizi hakutokea wakati
alipotakiwa kufika kwenye Kamati ya Uchaguzi kutoa utetetezi wake kuhusu
pingamizi.
(b) Pingamizi dhidi ya Ndg. Eliud P. Mvella
anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF
kupitia Kanda ya 7 (Iringa na Mbeya): Ndg. Mvella aliwekewa pingamizi na
Ndg. Said Kiponza, Ndg. Abu Changawa na Ndg. Peter Naminga, kwamba Ndg.
Mvella:
(i) Akiwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda hiyo ameshindwa kuleta maendeleo ya soka katika ukanda huo.
(j) Ana kesi ya rushwa katika mahakama ya wilaya ya Iringa
Kamati imeitupa pingamizi hiyo kwa kuwa haikukidhi
matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa
kutoambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya
pingamizi.
(c) Pingamizi dhidi ya Ndg. Epaphra Swai anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 3 (Shinyanga na Simiyu): Kamati ilijadili pingamizi zilizowasilishwa na Ndg. Ramadhani Sesso na Ndg. Tsotsie Chalamila, kwamba Ndg. Epaphra Swai:
(i) Alifanya ubadhilifu wa fedha alipokuwa Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA).
(ii) Alitumia madaraka yake vibaya alipokuwa MZFA kujinufaisha kwa kutumia MZFA.
(iii) Alivunja Katiba ya MZFA na FIFA
(iv) Anavuruga shughuli za uendeshaji mpira wa miguu mkoani Simiyu.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF ilipitia pingamizi hizo na ilijiridhisha kuwa
wawekaji pingamizi hawakuwa na sababu za msingi zilizoambatana na
vielelezo vinavyothibitisha maelezo ya pingamizi na kuwa pingamizi
zilizowasilishwa mbele yake zina chembechembe za wazi za mapatano ya
hila na udanganyifu (collusion) dhidi ya Ndg. Epaphra Swai. Kwa kutokidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) na hila/udanganyifu kwa Kamati, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imezitupa pingamizi hizo.
(d) Pingamizi dhidi ya Ndg. Vedastus F.K Lufano na Ndg. Mugisha Galibona wanaoomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 2 (Mwanza na Mara): Ndg. Lufano na Ndg. Galibona waliwekewa pingamizi na Ndg. Paul Mhangwa kwamba hawana uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu wa miaka mitano (5).
Kamati imeitupa pingamizi hiyo kwa kuwa haikuzingatia Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2).
(e) Pingamizi dhidi ya Ndg. Michael R. Wambura anayeomba kugombea nafasi ya Makamu wa Rais wa TFF: Pingamizi ziliwasilishwa na Ndg. Said Rubea Tamim na Ndg. Josea Samuel Msengi kwamba Ndg. Wambura:
(i) Alikiuka Katiba ya TFF kwa kuishitaki Klabu yake ya Simba mahakamani kuhusu masuala ya uchaguzi.
(ii) Alikosa uadilifu kwa kutumia kampuni yake binafsi kufanya biashara na Taasisi aliyokuwa aniongoza akiwa Katibu Mkuu wa FAT.
(iii) Amekuwa
akijaribu kupotosha umma kwamba vyombo vya TFF havifanyi kazi zake kwa
kutumia haki na kuviita ‘Mahakama za Kangaroo (Kangaroo Courts).
(iv) Mwaka
2004 alikiri kwamba alikuwa akiandikwa vizuri na vyombo vya habari kwa
kuwa alikuwa akivipa pesa na kwamba vyombo vya habari vilimgeuka kwa
sababu aliacha kuwapa waandishi pesa.
(v) Mwaka 2004 alikataa kutekeleza maagizo ya FIFA ya kutaka nafasi ya Katibu Mkuu wa FAT iwe ya kuajiliwa.
(vi) Alikosa uwezo wa kutekeleza wajibu na malengo ya TFF.
Ndg. Josea Samuel Msengi aliondoa pingamizi lake dhidi ya Ndg. Wambura. Kamati imelitupa pingamizi la Ndg. Said Rubea Tamim kwa kuwa halikukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2).
(f) Pingamizi dhidi ya Ndg. Jamal E. Malinzi anayeomba kugombea nafasi ya Rais wa TFF; Aliwekewa Pingamizi na Ndg. Agape Fue kwamba:
(i) Alivunja
Katiba ya TFF kwa kufanya jitihada kubwa za kuhakikisha kuwa wanachama
wa TFF kikiwemo Chama chake cha Mkoa wa Kagera haviheshimu wala
kutekeleza maagizo ya TFF, CAF, CECAFA na FIFA baada ya Kamati ya
Utendaji ya TFF kuwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba kwa njia
ya Waraka, ambayo yalihusisha pia maagizo ya FIFA na CAF
(ii) Hana sifa ya uzoefu wa miaka mitano katika uongozi wa mpira wa miguu.
(iii) Anakosa uadilifu na haiba ya kuliwakilisha Shirikisho nje na ndani.
Kamati imeitupa pingamizi ya Ndg. Agape Fue kwa kuwa mweka pingamizi hakutokea wakati alipotakiwa kufika kwenye Kamati ya Uchaguzi kutoa utetetezi wake kuhusu pingamizi hilo.
(g) Pingamizi dhidi ya Ndg. Athumani J. Nyamlani anayeomba kugombea nafasi ya Rais wa TFF: Ndg. Nyamlani aliwekewa pingamizi na Ndg. Mintanga Yusuph Gacha na Ndg. Medard Justiniani kwamba:
(i) Ni
Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Tanzania na kwa maana hiyo ni mtumishi
wa umma hivyo alikosa kigezo na sifa ya kugombea nafasi ya urais wa TFF.
(ii) Anakatazwa na Judicial Service Act, Public Service Act 2002 na Code of Conduct for Judicial Officers of Tanzania kugombea nafasi aliyoomba ya Rais wa TFF.
(iii) Kutakuwa na Mgoganao wa kimaslahi endapo Ndg, Nyamlani atachaguliwa kuwa Rais wa TFF.
(iv) Amekosa umakini na uadilifu kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake na kusababisha Akanunti za TFF kufungiwa na TRA.
Ndg. Mintanga Yusuph Gacha hakufika kutetea Pingamizi lake ni hivyo halikujadiliwa na Kamati. Kamati imelitupa pingamizi la Ndg. Medard Justiniani kwa
kuwa alishindwa kuithibitishia Kamati kuwa alikuwa na ufahamu wa
kutosha wa pingamizi lake ikiwa ni pamoja na viambatanisho vyake, hali
iliyotanabaisha kuwa pingamizi hilo lilikuwa na chembechembe nyingi za
hila na udanganyifu.
Angetile Osiah
KATIBU
KAMATI YA UCHAGUZI
No comments:
Post a Comment