![]() |
Mshambuliaji wa Manchester United Robin van Persie ameweka ujumbe kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwashukuru mashabiki wake walimtakia kheri katika siku yake ya kuzaliwa .
Nahodha huyo wa Uholanzi ametupia picha akiwa na watoto wake wawili pamoja na maputo mawili akionyesha namba 31 iliyowakilisha umri wa wake wa sasa na kuambatanisha ujumbe uliosomeka.
'Thanks everybody for all your
birthday wishes'.
Tofauti na wachezaji wengine maarufu wa Manchester, Van Persie alitengenezewa keki na wafanyakazi wa klabu hiyo.
Nahodha wa Uholanzi aliandaliwa keki ya kumtakia kheri siku ya kuzaliwa.
No comments:
Post a Comment