KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, July 29, 2012

HABARI ZA KIMATAIFA HII LEO: Ibrahimovic: Paris Saint-Germain ni bora kuliko AC Milan,Messi Apiga hat-trick na kuizamisha Raja Casablanca 8-0,Jack Wilshere kuwa nje mpaka October na nyingine.



Ibrahimovic: Paris Saint-Germain ni bora kuliko AC Milan

Zlatan Ibrahimovic ambaye ameanza kuitumikia timu yake mpya ya PSG anasema ameona mengi katika timu yake hiyo kiasi kusema ni bora kuliko Milan.
Amenukiliwa akisema Paris Saint-Germain ni bora kuliko timu yake ya zamani ya AC Milan.
Kufuatia mchezo mmoja wa hapo jana wa kirafiki dhidi ya D.C United ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 aliulizwa ni timu ipi bora kati ya timu yake ya sasa na ile ya zamani Ibrahimovic alijibu kuwa timu yake ya sasa ndio bora
Mapemwa mwanzoni mwa mwezi huu PSG ilifanya usajili muhimu (double swoop) kwa Ibrahimovic na mlinzi wa Kibrazil Thiago Silva ambao uliwagharimu wamiliki raia wa Qatari kiasi cha euro milioni 62.
 Kwasasa Silva yuko na kikosi cha Brazil kwenye michezo ya Olympic huku Ibrahimovic akiwa na PSG na jana akicheza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki dhidi ya D.C United ambapo alifinga bao lake la kwanza akiwa na timu hiyo katika dakika ya tatu ya mchezo.
 Kama ilivyokuwa kwa AC Milan timu ya zamani ya Ibrahimovic PSG pia alishindwa kupata taji lolote katika msimu wa 2011-12  lakini kwa kuwaongeza wachezaji wawili wa Milan pamoja na kiungo wa Pescara, Marco Verratti pamoja na mshambuliaji wa Napoli Ezequiel Lavezzi, Ibra amejenga matumaini makubwa kwa PSG.
Zote Milan na PSG ziko katika hatua ya makundi ya michuano ya vilabu bingwa ulaya 2012-13.
 

Montolivo akanusha hoja juu ya kuvurugika kwa AC Milan.

  Riccardo Montolivo amesisitiza kuwa AC Milan itaendelea kuwa moto licha ya kuhama kwa wachezaji wake muhimu kama Zlatan Ibrahimovic na Thiago Silva msimu huu.
Milan maarufu kama Rossoneri imeuza wachezaji wake muhimu kwenda Paris Saint-Germain mapema mwezi huu wa July huku wakongwe kama Gennaro Gattuso, Clarence Seedorf, Filippo Inzaghi, Gianluca Zambrotta na  Alessandro Nesta wakiachwa katika jaribio la kusuka upya kikosi cha timu hiyo.
Lakini pamoja na klabu hiyo kuchukua uamuzi huo bado  Montolivo ambaye ni miongoni mwa wachezaji wapya  ndani ya klabu hiyo anaamini kuwa San Siro itaendelea kuwa juu katika msimu mpya.
 Amenukuliwa na Gazzetta dello Sport akisema
"si dhani kama Milan iko kwenye shida kubwa kwa kufanya maamuzi hayo, ni kweli klabu imepoteza wachezaji muhimu Milan ni klabu kubwa kabla ya Ibrahimovic na Thiago na tutandelea kuwa hivyo hata bila ya wao."
 
Messi Apiga hat-trick na kuizamisha Raja Casablanca 8-0

 Lionel Messi ameanza tena shughuli yake ya kupiga ‘hat-trick’  akiwa na kikosi chake cha Barcelona baada ya kuchapa bao 8-0 Raja Casablanca ya Morroco katika mchezo wa kirafiki kule Grand Stade mjini Tangier.
Alexis Sanchez alianza kufunga bao la kwanza kabla ya  Messi kupiga mawili. Wawili hao wakaendelea kuinyanyasa Raja Casablanca huku Messi akiendelea kufanya kazi yake kuifanya Barcelona kuongoza kwa mabao 4-0 na Messi akikamilisha hat-trick wakati wa mapumziko.
Dani Alves naye alifanikiwa kufunga na kuingia kwenye kitabu cha mabao akifunga bao la penati kunako dakika ya 58 kabla ya nyota vijana Sergi Roberto na Gerard Deulofeu kuongeza mengine mawili katika dakika tatu za mwisho za mchezo.

 Baada ya mchezo bosi mpya wa Barcelona Tito Vilanova amempongeza Messi katika mchezo wake huo wa  kwanza wa matayarisho ya kunza kwa msimu mpya  kufuatia kukosekana katika mchezo wa kwanza dhidi ya Hamburg uliofanyika jumanne.
Amenukuliwa Vilanova akisema
"unapokuwa na mchezaji bora wa dunia mwenye uwezo mkubwa wa kufunga huo anaonyesha tofauti, na kwa mara nyingine tena ameonyesha hilo,"
 "mchezo huu ulikuwa mzuri kwasababu tumecheza na timu ambayo inakimbiza na hata wachezaji vijana wamecheza vizuri usiku huu."
Messi mwenyewe akiongea na El Mundo Deportivo amesema
"kwa muda mrefu sijapata kucheza mchezo wa matayarisho ya msimu kutokana na kuchelewa kufika kwangu ilikuwa ni fursa nzuri kwani nimetoka katika mapumziko ya muda mrefu.


Rodgers: Carroll anataka kusalia 

 Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amesisitiza kuwa  Andy Carroll ni mwenye furaha na anataka kuendelea kusalia Liverpool na anataka kuzoea aina mpya ya mchezo ambao unafundishwa katika klabu hiyo yenye maskani yake Anfield.
Kwasasa kumekuwepo na tetesi kuwa Carroll huenda akaondoka Liverpool baada ya kuhangaikia kusaka nafasi ya kucheza tangu kujiunga kwake na klabu hiyo akiatokea Newcastle United kwa ada ya pauni milioni £35 mwezi januari 2011.
Klabu yake ya zamani imekuwa katika harakati za kumrejesha carroll st james' park lakini mpango huo ulikataliwa na wekundu hao wa london.
West Ham pia imetenga pauni milioni £2 kumchukua  Carroll kwa mkopo mpaka kumalizika kwa msimu wa 2012-13 lakini pia kwa mpango wa kudumu wa pauni milioni £16 ikiwa klabu hiyo itaepuka balaa la kushuka daraja.

Lakini Rodgers bado anamtaka mshambuliaji huyo kuendelea kutoka mchango wake katika timu hiyo na jana akiingia akitokea benchi katika mchezo wa kujiandaa na ligi dhidi ya Tottenham uliomalizika kwa sare ya bila kufungana.

Jack Wilshere kuwa nje mpaka October

 Kocha wa Arsernal  Arsene Wenger amesema Jack Wilshere hatakuwa dimbani akitoa huduma katika klabu hiyo mpaka mwezi  October.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20 wa England alikosekana katika msimu mzima wa 2011-12 akisumbuliwa na na ankle na alifanyiwa upasuaji mdogo mguu mwezi May mwaka huu.
Amenukuliwa Wenger baada ya mchezo wa mwisho wa ziara yao ya barani Asia akiwa katika jiji la Hong Kong akisema
 "tunaimani ya kuwa tena Wilshere mwezi October,"
"na kwa kuwa Abou Diaby amerejea , itakuwa ni kama tumesajili wachezaji wawili wapya. Kikosi kitakuwa shupavu na kimashindano."
Wilshere alipatwa na ankle kiangazi mwaka uliopita na amefanyiwa upasuaji wenye mafanikio na mwenyewe ana matumaini kuwa katika nafasi ya kuanza mazoezi mepesi mwezi August lakini katika hali nzuri mwezi October.

No comments:

Post a Comment