KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, July 29, 2012

SIMBA YATOSA MICHUANO YA SUPER 8



Geofrey Nyange kaburu
Baada ya shirikisho la soka Tanzania Tff kuingia mkataba wa miaka mitatu na benki ya BancABC  Juu ya kuanzishwa kwa michuano mipya itakayoshirikisha jumla ya timu nane uongozi wa klabu ya simba umelishangaa shirikisho hilo  kwa kukurupuka bila  kushirikisha vilabu husika .
TFF ilitangaza kuwa kuanzia August 4 mpaka 18 timu bora tatu za bara na tatu za Zanzibar pamoja na timu moja moja zilizopanda daraja msimu huu kucheza ligi kuu kwa pande zote mbili Zanzibar na bara zitashiriki michuano hiyo iliyopewa jina la BancABC SUP8R soccer Tournment 2012.
Makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu’ akiongea na Rockersport.com amesema pamoja na kupokea barua kutoka TFF juu ya kuwepo kwa mashindano hayo , klabu yake imeshaliandikia barua shirikisho hilo wakiwapa masharti ili waweze kushiriki michuano hiyo huku akionyesha kutokuwa tayari kushiriki mashindano hayo .
Kaburu amesema moja ya masharti hayo ni kutaka TFF  ikutane na vilabu husika kabla ya kuanza kwa mashindano hayo kwa kusema inashangaza TFF imeingia mkataba binafsi bila walengwa kushirikishwa.
Akiendelea zaidi kaburu amesema katika barua waliyopokea TFF inaeleza kuwa vilabu vitaambulia asilimia 25 ya mgawo wa mapato huku TFF wakiondoka na asilimia 50.
Ameshangaa kwa kuuliza kuwa inakuwaje michuano yenye udhamini TFF wajichotee asilimia kubwa lakini pia akashangaa kulikoni wao kama watangazaji wa biashara ya wadhamini wakapata mgawo mdogo,
Kama haitoshi Kaburu amesema  michuano hiyo inaonekana haina tija kwa sababu ni mshindi wa kwanza pekee anayepata zawadi huku zingine zikiwa hazina kitu.
Amesema endapo TFF itashindwa kukutana na vilabu na kuzungumzia michuano hiyo na masuala mazima ya maslahi kwa vilabu husika Simba kamwe haiwezi kushiriki.
Mbali ya hivyo Kaburu amedokeza kuwa ukiangalia kwa undani michuano hiyo imeibuliwa tu kwa sababu haipo kwenye kalenda ya TFF lakini kama haitoshi akaongeza kuwa Simba tayari wameshashiriki michuano ya aina mbili kwa sasa walianza na michuano ya ujirani mwema  wakawa mabingwa na kisha wameshiriki michuano ya Kagame ambapo wametolewa katika hatua ya robo fainali na Azam ,
Kaburu ameongeza kuwa kiufundi si vizuri kushiriki michuano  ndani ya michuano hali inayopelekea timu kutokuwa nzuri na kwenda tofauti na program ya kocha wao.
TFF imezitaja timu za Simba, Yanga , na Azam pamoja na timu moja iliyopanda daraja la kwanza kushiriki michuano kama ilivyo kwa upande wa Zanzibar.
Michuano hiyo imepangwa kwa mtindo wa makundi mawili na itachezwa kwenye miji ya Dare s salaam, Mwanza , Arusha na Zanzibar.

No comments:

Post a Comment