![]() |
Gonzalo Higuain |
Gonzalo
Higuain anajipanga kuingia mkataba mpya na Real Madrid kufuatia mkutano baina ya baba
yake,wakala na mkurugenzi wa Madrid Jose Angel Sanchez mkutano uliofanyika Santiago
Bernabeu.
Kwasasa Higuain
nyota wa kimataifa wa Argentina yuko katika mkataba na Madrid utakao malizika
kiangazi 2016, lakini bado Los Blancos wanataka kumaliza kabisa fununu na
uwezekano wowote nyota huyo kupata mawenge ya kuondoka na wanampango wa
kumuongezea mashahara euro milioni €3.5 kwa msimu mpaka euro €4.5m.
Alijiunga na
Real Madrid akitokea River Plate January 2007, na tangu wakati huo amefunga
jumla ya magoli 91 katika ligi kuu ya nchini Hispania La Liga baada ya kucheza
mechi 162.
No comments:
Post a Comment