Zambia imempa idhini kocha Herve Renard kuyaacha
majuku yake katika timu ya taifa ya nchi hiyo ili kuchukua jukumu lake
jipya la kuwa kocha wa timu ya ufaransa ya FC Sochaux.
Kocha huyo alikuwa ameanza muhula wa pili wa
mkataba wake kuwa kocha wa timu ya taifa ya Zambia mnamo mwezi Oktoba
mwaka 2011 na kuiwezesha Chipolopolo kufuzu kwa kombe la mataifa ya
Afrika miezi minne baadaye.
Lakini Zambia ilikuwa na wakati
mgumu mwaka huu kiaso cha kubanduliwa nje ya mechi za kufuzu kwa kombe
la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Zambia sasa imempa kazi ya muda Patrice Beaumelle kuwa kocha wa Chipolopolo.
Beaumelle, amekuwa akifanya kazi kama kocha wa
muda, na atashikilia wadhifa wa kocha mkuu wakati Chipolopolo
watapocheza mechi ya kirafiki na Brazil mjini Beijing tarehe 15 Oktoba.
Shirikisho la soka nchini humo katika taarifa
yake lilisema kuwa kocha "Herve Renard ameachishwa majuku yake ili
kumruhusu kuiongoza timu ya Ufaransa.''
Renard, mwenye umri wa miaka 45, alichukua
wadhifa huo wa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Zambia mwaka 2008 na
aliiongoza timu hiyo hadi kufika robo fainali za kombe la mataifa ya
Afrika mwaka 2010.
Baadeya alikuwa kocha wa timu ya Angola na USM
Alger kwa muda kabla ya kurejea kuwa kocha wa Zambia na kutimiza ndoto
yake ya kuiongoza Zambia kunyakua kombe la taifa bingwa Afrika mwaka
2012.
No comments:
Post a Comment