KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, January 12, 2013

MATAYARISHO YA BONANZA LA WACHEZAJI WAZAMANI YAKAMILIKA KUFANYIKA KESHO UWANJA WA SIGARA CHANG'OMBE.

 Jumla ya timu 9 zinazowakilisha timu za wachezaji wa zamani waliowaji kutamba katika ligi kuu ya soka Tanzani bara zamani ikiitwa ligi daraja la kwanza zimethibitisha kushiriki Bonanza hilo huku matayarisho yakiendelea katika dakika za mwisho.

Akiongea na Rockersporta mratibu wa Bonanza hilo lililodhaminiwa na benki ya NMB Kennedy Mwaisabula mzazi amesema kila kitu kiko katika mstari ambapo amewataka wachezaji wa timu zote kufika mapema kwani michezo hiyo itaanza saa mbili asubuhi.
 Timu za Yanga, Coast na Tukuyu stars 
ambazo hazikuwepo katika bonanza la mwezi Novemba zimesema iko katika mazingira mazuri ya ushiriki wao na kwamba wanatarajia kutoa upinzani katika bonanza la kesho.

Timu zitakazo shiriki ni pamoja na Simba, Yanga, Plisner, Tukuyu, Reli ya Morogoro, Bandari Mtwara, Kariakoo ya Lindi, Coast na Milambo ya Tabora.

No comments:

Post a Comment