KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, January 13, 2013

RAIS SHEIN WA ZANZIBAR AZINDUA MRADI WA ONE WORLD FOOTBALL NA KUTAKA MICHEZO IRUDI MA-SCHOOL. NAO AZAM WATETEA TAJI LA MAPINDUZI.

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein amezindua Mradi wa Soka wa 'One World Football'  na kuwataka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kurejesha michezo Mashuleni.

 Akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo uliofanyika kwenye uwanja wa Amani mjini Zanzibar ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Shein amesema kuwa mradi huo una umuhimu mkubwa katika kuinua sekta ya michezo kwa vile mipira 20,000 yenye thamani ya milioni 800 itatolewa bure katika vituo vya yatima, mashuleni na vilabu vya michezo zikiwemo timu za mitaani katika visiwa vya Unguja na Pemba.

 Aliongeza  kuwa michezo haimzuii mtoto kutoweza kusoma na kufanya vizuri darasani bali humpelekea mtoto kuweza kufahamu na kufanya vizuri kwenye masomo yake kwa kuwa michezo inaweza kumjenga kiakili.

 Dk. Shein alisema kuwa amefarijika kusikia kuwa mradi huo una azma ya kusaidia kuleta hamasa na vuguvugu la shughuli za michezo hasa kwa mpira wa miguu, netiboli pamoja na kuinua vipaji ambavyo baadae vitaendelezwa ili kupata wachezaji wazuri nchini.

 Ipo  haja ya kurejesha taratibu za kutilia mkazo na kuziimarisha timu za watoto mashuleni na pia timu za vijana mitaani na kuziandalia mashindano mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuzipa nguvu ligi za ‘Juvenile, Junior na Central’.

Alisisitiza kuwa mashindano ya madaraja hayo ndiyo msingi wa kuandaa timu kama ilivyokuwa siku za nyuma na kuweza kupata wachezaji wazuri kama ilivyo kwa timu kubwa Duniani ambao uwekeza kwa vijana.

"Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) kisimamie jambo hili na kuwa na programu endelevu na ratiba ya uhakika ili kuweza kuibua vipaji na kuviendelea katika mchezo wa soka," alisema Dk Shein.

Aidha, aliitaka Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo kufanya jitihada maalum za kufufua na kuimarisha michezo mingine hususani mchezo wa mpira wa magongo (hockey), criket na mbio za baskeli ambazo ziliipatia umaarufu na sifa kubwa Zanzibar.

Mapema Waziri wa Wizara ya Habari, Said Ali Mbarouk, alisema kuwa lengo kubwa la mradi huo ni kuhakikisha watoto nao wanapata fursa na nafasi ya kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii ikiwemo michezo.

Alisema kuwa mipira itakayolewa katika mradi huo itasambazwa nchini kote hadi vijijini na itatolewa bure bila ya malipo yoyote na imetolewa msaada na Kampuni ya Magari ya Chevrolet ambao ndiyo wafadhili wa mradi huo kwa kushirikiana na Shirika la kupigania haki za watoto la Kimataifa la 'Save the Children'.

Mkurugenzi wa One World Football Kanda ya Afrika Sandra Cress alitoa pongezi kwa Zanzibar kwa kuweza kufanikisha Mradi huo kwa wakati muafaka.

Alisema kwamba mradi huo utasadia kuibua vipaji vya watoto pamoja na kuwapa haki watoto hasa vijijini ya kushiriki michezo.
        


KOMBE LA MAPINDUZI.
Katika hatua nyingine timu ya Azam Fc ya Chamazi jijini Dar es Salaam ambayo pia ndio wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho imefanikiwa vema kutetea taji lake la michuano ya Mapinduzi baada ya kufaniwa kuicha Tusker ya kenya kwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliofanyika katika uwanja wa Amani mjini Zanzibar.
 Tusker ndio waliokuwa wa kwanza kuandika bao lililofungwa la kuongoza lililowekwa nyavuni na Michael Were kunako dakika ya 60 kipindi cha pili kabla ya Azam kusawazisha kwa bao la penati lililofungwa na Joakins Atudo baada ya Luke Ochieng kuunawa mpira katika eneo la hatari.
 
mpaka dakika 90 mabao yalikuwa 1-1, na ndipo katika dakika za 30 za nyongeza Azam kupitia kwa Gaudience Mwaikimba wakafanikiwa kuandika bao la ushindi dakika ya pili tu ya muda wa nyongeza.
 
Azam imezawadiwa shilingi milioni 10 kwa kutwaa taji hilo, nao Tusker wakiambulia shilingi za kitanzania milioni 5 kwa kushinda nafasi ya pili.

No comments:

Post a Comment