Timu ya Young Africans leo asubuhi imemaliza
mazoezi yake kwa kufanya mazoezi ya
kujenga mwili na uimara (Gym) iliyopo katika hoteli ya Fame Residence leo
asubuhi na yakiwa ndio mazoezi ya mwisho katika kambi ya mafunzo ya wiki mbili
iliyokuwa ikiendelea katika viwanja vya Fame Residence Football mijini Antlaya.
Kocha mkuu
Ernest Brandts akishirikiana na Fred Felix Minziro na Razaki Siwa leo
waliongoza mazoezi ya Gym kuanzia majira ya saa tatu na nusu asubuhi mpaka
majira ya saa saa tano na nusu asubuhi ambapo baada ya mazoezi hayo wachezaji
wamepewa nafasi ya kupumzika kujiandaa na safari ya hapo kesho kurudi Tanzania.
Akiongelea michezo ya kirafiki mitatu
waliocheza na timu za Armini Bielefeld, Deinizlispor na Emmen Fc kocha mkuu wa
Yanga Ernest Brandts amesema michezo ilikuwa ni mizuri na wamepata nafasi ya
kuona mapungufu machache yaliyojitokeza na anaamini watayafanyia kazi na
kuendelea kufanya vizuri.
Tumecheza michezo mitatu, wa kwanza tulitoka
sare na Amrinia Bielefeleld, mchezo ulikua mzuri na timu yangu ilicheza vizuri
kwa dakika 90 zote za mchezo licha ya
Arminia kusawaisha bao dakika za lala salama huku mwamuzi aklishindwa kutoa
maamuzi sawa na mshika kibendera wake, ambapo mfungaji alikua maeotea.
Mchezo wa pili dhidi ya Denizlispor nao pia
timu ilicheza vizuri na kuweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini
umakini wa washambuliaji ulitukosesha ushindi kwani Tegete alitumia nafasi
aliyoipta kufunga bao la mapema kabla ya Waturuki hawajasawazisha kwa bao la
utata kisha kupewa penati ya utata pia.
Mchezo wa mwisho dhidi ya Emmen FC ulikuwa
mzuri pia na kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza tuliutawala mchezo na kupata
nafasi kadhaa za kufunga mabao lakini kutokua makini wa washambuliaji wetu pia
kulichangia sisi kukosa ushindi, kabla ya kipindi cha pili Emmen FC kucharuka
na kupata mabo mawili ya haraka haraka kutokana na uzembe wa walinzi na mlinda
mlango Yusuph Abdul.
Tunaushukuru uongozi kwa kukubali kutupa
nafasi ya kuweka kambi Uturuki, tumkeaa pamoja kwa mda mrefu huku tukitoka
mafunzo kwa vitendo, vifaa na mahitaji yote vikiwepo ,kukiwa na hali ya
utulivu, kifupi tumejifunza mambomengi sana ya msingi ambayo yatatusaidia
kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom na mashindano
yatakayotukabili alisema 'Brandts'
Ally Mustafa 'Barthez, na Nizar
Khalfani wakifanya mazoezi ya Gym leo asubuhi katika hoteli ya Fame Residence.
|
No comments:
Post a Comment