Ferguson: Suarez anapenda kuzongwa
zongwa.
Kuelekea katika
mchezo wa kesho dhidi ya Liverpool hapo kesho, meneja wa mashetani wekundu Sir Alex
Ferguson anaamini Luis Suarez ni mtu ambaye anapenda kuzingirwa na mizozo.
Suarez atakuwa
akiikabili United katika uwanja wa Old Trafford hapo kesho kwa mara ya kwanza
tangu alipogomea kupenea mkono na Patrice Evra mwezi February mwaka jana.
Tukio
hilo ni moja kati ya mlolongo wa matukia yanayo muhusu mshambuliaji huyo ambayo
yamekuwa yakiibua gumzo kubwa.
Mruguay huyo
kwa mara nyingine aliingia katika mjadala wiki hii pale alipofunga goli dhidi Mansfield
mchezo wa michuano ya FA goli ambalo lilithibitika wazi kuwa kabla ya kufunga
alitumia mkono kuutengeneza mpira kabla ya kupiga kwa mguu wake wa kulia na
kutumbukiza wavuni.
Sir Alex Ferguson
anadai kuwa hakushangazwa na Suarez kuingia katika gumzo lingine kubwa kama
hilo.
Amenukuliwa akisema
"Sikuangalia
mchezo dhidi ya Mansfield, hivyo ni vigumu kusema kama ilikuwa ni makusudi ama
hapana".
"lakini
nadhani huyu kijana amekuwa ni mtu wa kuzongwa zongwa sasa sijui kama
anafurahia hiyo au laa."
Benitez amtetea Torres.
Rafael
Benitez amemtetea mshambuliaji wake Fernando Torres wakati ambapo kumejitokeza
ukosoaji mkubwa kwa mshambuliaji huyo raia wa Hispania na anaamini kuwa
mshambuliaji huyo atafanikiwa kuwashinda mashabiki wakosoaji wake wa klabu yake ya Chelsea.
Torres mwenye
umri wa miaka 28, ameifungia Chelsea magoli 14 msimu huu lakini kiwango kibovu
katika mchezo dhidi ya Swansea mchezo wa michuano ya Capital One kimeibua
maswali mengi juu ya nafasi yake katika timu.
Kuongezwa kwa
Demba Ba kikosini ambaye alifunga magoli mawili kati ya matano katika mchezo wa
michuano ya FA dhidi ya Southampton ambapo Chelsea ilishinda 5-1 kumeibua
shinikizo jipya kwa mshambuliaji wengi wakitaka akazane zaidi, lakini hata hivyo Benitez
amemtetea Torres kwa kusema kuwa alikuwa anaumwa siku ya mchezo dhidi ya Swansea.
Mancini anamatumaini ya kumsajili
tena Tevez.
Roberto
Mancini amesema anatarajia klabu yake ya Manchester City itampa mktaba mpya mshambuliaji muargentina Carlos Tevez.
Mkataba wa
sasa wa Tevez utamalizika katika kipindi cha kiangazi mwaka 2014.
Kwasasa City haiko tayari
kumpoteza mchezaji ambaye aliwagharimu ada ya uhamisho ya pauni milioni £25 ndani
ya kipindi cha miezi 18.
Hali hiyo moja
kwa moja itamzuia Roberto Mancini kupata mchezaji mbadala yake kwani sheria ya
udhibiti wa matumizi ya shirikisho la soka Ulaya EUFA zinawazuia kufanya hivyo
kwakuwa wanatakiwa kuweka sawa mzani wao wa matumizi katika vitabu vyao na kwamba wanatakiwa kuuza kabla ya kununua.
Hiyo pia
inaangaliwa kama ni ujenzi mpya wa mahusiano mazuri baina yao, tangu kipindi
kile ambacho Tevez alipogomea kufanya mazoezi ya kupasha misuli moto kabla ya kuingizwa
uwanjani katika mchezo wa michuano ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich
mwezi September 2011 ambapo alikaririwa Manchini akisema mchezaji huyo
amejimaliza.
Hali hiyo
ilipelekea Tevez kupoteza pauni milioni £9.3 kama makato yaliyotokana na sehemu ya mshahara
wake na bonasi nyingine sambamba na kukalia benchi kwa miezi sita kabla ya
kurudi na kuisaidia City kushinda taji la ligi kuu ya England.
Steven Gerrard apinga sera ya meneja wake.
Nahodha wa Liverpool
Steven Gerrard ameonya mpango wa meneja wake Brendan Rodgers wa kutaka
kuwatumainia zaidi vijana katika kipindi cha mapinduzi makubwa ya Anfield.
Tangu
kuwasili kwa Rodgers kiangazi mwaka jana, wekundu hao wamekuwa na mpango wa
kuwasajili zaidi wachezaji vijana na tayari imefanya hivyo kwa Joe Allen, Fabio
Borini na Daniel Sturridge ambao wote bhawajafika umri wa miaka 24.
Steven Gerrard na McAllister mwaka 2000. |
Gerrard
ambaye kwasasa ana umri wa miaka 34, hana imani kama sera hiyo kama itaivusha Liverpool
kuelekea kwenye mageuzi yanayotakiwa hivi sasa, ikiwa kwasasa iko katika nafasi ya nane
katika msimamo wa ligi ya ‘Barclays Premier’ hivyo ni vigumu kwa sera hiyo kuirejesha katika changamoto ya michuano mikubwa ya vilabu ulaya kama klabu bingwa.
Kiungo huyo
ametolea mfano usajili wa Gary McAllister ambaye alisajiliwa Anfield akiwa na
umri wa miaka 35 mwaka 2000 kuwa ulikuwa ni mpango wa maendeleo na kwamba itakuwa
vizuri kama kutakuwa na mchanganyiko wa umri katika kikosi.
Amenukuliwa akisema,
'Sikubaliani
na sera hiyo kiukweli'.
'nimeona
usajili mwingi duniani kote watu wanasajili umri wa miaka 28, 29na pengine
zaidi ya hapo na wanafanya kazi nzuri kwa kweli. Sitaweza kuielewa sera hii japokuwa ni
kweli kila mtu anataka wachezaji vijana wenye akili Waingereza lakini si kwa
asilimia 100.
Kuelekea fainali za mataifa ya Afrika 2013
Asamoah Gyan anasema ni usia wa mama yake asipige tena penati katika timu ya taifa.
Nahodha wa
timu ya taifa ya Ghana Asamoah Gyan ameweka wazi msimamo wake kuwa hayuko
tayari kupiga penati katika muda muda wa kawaida katika michezo ya mataifa ya
Afrika inayotarajiwa kuanza nchini Afrika Kusini januari 19.
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 27 alikosa penati ambayo pengine ingeipeleka Ghana kwenye
husu fainali ya kombe la dunia mwaka 2010 na katika nusu fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika mwaka jana.
Baada ya
kupata usumbufu mkubwa wa matusi na mengine akitukaniwa mama yake kutoka kwa mashabiki, matusi ambayo yalimfanya
apumzike kuichezea timu ya taifa , Gyan amerejea huku akitoa tamko la wazi
kabisa kuwa hatapiga mpira wowote wa penati katika fainali hizi.
Amenukuliwa akisema
"nimeamua
kutokupiga penati katika timu ya taifa".
"wachezaji
wengi wakubwa wamekosa penati Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Diego Maradona wote
wachezaji wakubwa na katika siku mbaya inaweza kutokea.
"lakini
kama nilivyosema mwezi uliopita sitapiga tena penati. Kabla mama yangu hajafa
mwezi November aliniambia nisipige tena penati."
No comments:
Post a Comment