KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, August 22, 2013

Wenger sasa anakula tena matapishi yake anamrejesha Flamini baada ya kutemwa na Milan.

Mathieu Flamini
Mathieu Flamini enzi hizo.
Mathieu Flamini
Aliichezea Arsenal zaidi ya michezo 100 , Flamini aliihama Arsenal na kujunga na AC Milan mwaka 2008

 Siku 12 za marekebisho ya kikosi cha Arsene Wenger zinaonekana kuelekea pazuri kwani taarifa zinasena kuwa Arsenal huenda ikapata mkataba na Mathieu Flamini, ikiwa ni miaka mitano baada ya mchezaji huyo kuihama klabu hiyo na kujiunga na AC Milan.

Milan ilimuacha kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 mwishoni mwa msimu na tangu wakati huo amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha Wenger katika kipindi cha wiki mbili sasa.

Meneja wa Arsenal amekuwa akivutiwa na Flamini na anataka kumpa mkataba ambapo inaarifiwa kuwa Flamini licha ya kuwepo na hali ya kutakiwa na vilabu vingine.

Huo utakuwa ni usajili wa pili kwa Wenger ambapo utakuwa ni usajili wa pili huru na usajili wa wanne kwa wachezaji wake wa zamani kurejea kikosini kwani alikwisha kufanya hivyo huko kwa akina Sol Campbell, Jens Lehmann na Thierry Henry (mara mbili) ambao walirejea Emirates.

Usajili wa Flamini huenda ukakamilishwa kesho na huenda akawepo dimbani katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Fulham.
Thierry Henry
Arsenal old-boy: Thierry Henry alitangazwa kurejea wakati mwaka 2012 ambapo alifunga goli klatika michuano ya FA dhidi ya Leeds i2012.

Sol Campbell
Jens Lehmann

Jens Lehmann na Sol Campbell pia walirejea kwa Arsene Wenger baada ya kuwa uhamishoni London ya kaskazini.

Flamini alijiunga na kikosi hicho cha Italia cha Milan lakini alisumbuliwa na hali ya ubora wa afya yake ikiwa ni pamoja na kupatwa na matatizo ya mguu matatizo ambayo yalimuweka n je ya uwanja kwa msimu mzima wa 2011-12.
Wenger anaimani kuwa kurejea kwa Flamini kutarejesha uzoefu baada ya kukabiliw na majeruhi na wengine kadhaa kuondoka kikosini.
Viungo Mikel Arteta, Abou Diaby na Alex Oxlade-Chamberlain wote ni majeruhi.
Mathieu Flamini
Flamini kutoka San Siro narejea tena Arsenal.

Laurent Koscielny
Laurent Koscielny jana alijeruhiwa

No comments:

Post a Comment