KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, November 25, 2013

Zambia Shipolopolo yaungana na Ghana na Nigeria kucheza kombe la dunia.


Zambia imefanikiwa kwa mara ya kwanza kutinga fainali ya kombe la dunia kwa wanawake wenye umri chini ya miaka 17 fainaliambazo zitafanyika Costa Rica 2014.

Timu hiyo maarufu kama Shepolopolo imeungana na Ghana na Nigeria wakiwa wawakilishi wa Africa kwenye fainali hizo za dunia.
Hii ni mara ya kwanza kwa timu hiyo ya wanawake kufikia hatua hiyo ikipata nafasi yake baada ya kuwararua wapinzani wao wakubwa wa ukanda Afrika kusini kwa mabao 3-1 katika mchezo wa mkondo wa pili uliopigwa Jumapili mjini Johannesburg.

Ushindi huo kupitia mabao ya Grace Chanda na Irene Lungu umeipa Shipolopolo ushindi wa jumla wa mabao 6-4 kufuatia sare ya mabao 3-3 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Lusaka.

Fainali ya dunia itapigwa kuanzia Machi 15 na kumalizika Aprili 5 mwakani nchini Costa Rica.


No comments:

Post a Comment