KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, November 25, 2013

CAF yaweka ukomo wa kuthibitisha ushiriki wa michuano ya vilabu.

Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limetangaza tarehe ya mwisho kwa wanachama wake kuthibitisha ushiriki wa vilabu vyao katika michuano ijayo ya vilabu barani humu kuwa ni Novemba Novemba 30 2013.

CAF imetaka vyama vyote vya soka ambavyo ni wanachama wake vinapaswa kuthibitisha ushiriki wa vilabu vyao (CAF Interclubs competitions (Orange CAF Champions League and Orange CAF Confederation Cup) kwa msimu wa 2014.

Chama chochote ambacho kinataka kushiki katika michuano hiyo wanapaswa kuwasilisha katika sekretarieti ya CAF maombi yao ambayo yataambatana na ada ya kujiunga ya dolari za kimarekani $300, na kwamba maombi hayo yanapaswa kutumwa CAF kwa barua pepe au  fax si zaidi ya Novemba 30 2013.

Kuhusu usajili wa wachezaji, orodha kamili ya wachezaji wasiozidi 30 inapaswa kuwasilishwa sekretarieti ya CAF kabla ya Desemba 31 2013. Orodha hiyo inaweza kufanyiwa marekebisho lakini baada ya Januari 15 hakutakuwa na marekebisho ya aina yoyote ikiwa ni pamoja na kubadilisha wachezaji.

No comments:

Post a Comment