KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, November 25, 2013

Stephen Keshi: Siogopi kufukuzwa kama huko nyuma kuelekea kombe la dunia.

Kocha wa kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria Stephen Keshi amesisitiza kuwa haogopi kufukuzwa kazi kabla ya fainali ya kombe la dunia 2014 nchini Brazil.
Chini ya Keshi Nigeria imefanikiwa kupata tiketi ya kucheza kombe la dunia baada ya ushindi wa jumla wa mabao 4-1 dhidi ya Ethiopia mchezo wa hatua ya mwisho ya mtoano.
Mara mbili nahodha huyo wa zamani wa Super Eagles amekuwa akizikosa fainali baada ya kampeni ya mafanikio ya kufuzu.
Mwaka 2002 Keshi alikuwa msaidizi wa Shuaibu Amodu wakati Nigeria ilipofuzu kombe la dunia lakini wawili hao walifukuzwa kazi na nafasi zao kuchukuliwa na Adegboye Onigbinde kabla ya fainali kupigwa Korea Kusini na Japan.
Miaka minne baadaye Keshi alikutana na kadhia kama hiyo ya kufukuzwa kuelekea kwenye fainali ya mwaka 2006 nchini Ujerumani licha ya kuongoza kikosi mpaka kufikia fainali kwa mara ya kwanza na sasa inatazamwa kama wakati wa kurejesha kumbukumbu nyuma. 

 Amenukuliwa Keshi akisema
“Sihitaji msaidizi kutoka nje kuifanya Super Eagles ifanye vema kombe la dunia
"kazi hii ni ya kuajiriwa na kufukuzwa " 
"nilipokfukuzwa mwaka 2002 ilikuwa kwangu mshituko lakini haya ni maisha, sawa yote yamepita kwani huwezi kuendelea kuishi na hasira na kukata tamaa.
"Tunazungumzia juu ya Nigeria hapa, hivyo huwezi juu nini kitatokea.
"lakini kilichomuhimu kwasasa ni kwamba tunaangalia zaidi kilichombele ambacho ni kuandaa wachezaji wangu na si kitu kingine.

No comments:

Post a Comment