Kocha wa timu ya taifa ya Zambia Patrice Beaumelle ametangaza kikosi cha wachezaji 20 kwa ajili ya michuano ya Cecafa challenge Cup 2013 itakayofanyika nchini Kenya.
Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji 12 ambao walikuwa ni sehemu ya wachezaji walioshiriki michuano ya Cosafa Cup 2013 mwezi Julai nyumbani na ambao walicheza fainali dhidi ya Zimbabwe huko Ndola na kikosi hicho kinajumuisha mchezaji mmoja tu anayecheza soka nje ya nchi hiyo Kabaso Chongo ambaye anaichezea TP Mazembe ya DR
Congo.
Kiungo wa Green Buffaloes Felix Katongo ndio jina pekee lililozoeleka ndani ya kikosi cha Chipolopolo pamoja na mlinda mlango wa Power Dynamos Joshua Titima.
Wachezaji wawili muhimu wameachwa kutokana na kuwa majeruhi ambao ni mlinda mlango wa Arrows Daniel Munyau na nyota mwingine wa klabu hiyo Bruce Musakanya.
Zambia inashiriki kama timu mualikwa katika michuano hiyo ya Cecafa ambayo itafungua pazi Novemba 27 hadi Desemba 12 jijini Nairobi.
Kikosi cha Beaumelle kipo katika kundi B pamoja na Burundi, Somalia na Kilimajaro stars ambao wataanza kutupa karata yao ya kwanza Novemba 28 katika uwanja wa Machakos.
Zambia ilishinda kwa mara ya mwisho taji hilo mwaka 1991 walipoichapa Kenya 2-0 katika fainali iliyofanyika nchini Uganda.
Kikosi kamili cha Zambia
Goalkeepers: Joshua Titima (Power Dynamos), Toaster Nsabata (Nchanga Rangers)
Defenders: Jimmy Chisenga, Bronson Chama (Red Arrows), Christopher
Munthali (Nkana), Kabaso Chongo (TP Mazembe, DR Congo), Salulani
Phiri(Zanaco)
Midfielders: Kondwani Mtonga (Zesco United) Roderick Kabwe (Zanaco),
Misheck Chaila (Konkola Blades), Julius Situmbeko, Mathews Nkowani
(Power Dynamos), Sydney Kalume (Nkana), Felix Katongo (Green Buffaloes),
Justin Zulu (Kabwe Warriors)
Strikers: Reynold Kampamba, Festus Mbewe (Both Nkana), Alex Ng’onga ,
Bornwell Mwape (Nchanga Rangers), Stanley Nshimbi (Red Arrows)
No comments:
Post a Comment