Kocha wa kikosi cha timu ya taifa ya Rwanda 'Amavubi Stars' Eric Nshimiyimana ametangaza kikosi cha mwisho cha wachezaji 20 kwa ajili ya michuano ya GOtv Cecafa Senior Challenge Cup ambayo imepangwa kuanza kutimu vumbi Novemba 27 hadi Desemba 12 nchini Kenya.
Kiungo wa zamani wa Proline Andrew Buteera amejumuishwa kikosini ilhali nyota mwenziye wa zamano na winga wa SC Victoria University Charles Tibingana akikosa nafasi ndani ya kikosi hicho.
Rwanda ipo katika kundi C sambamba na mabingwa watetezi wa taji hilo Uganda, Eritrea na Sudan na wanatarajiwa kuanza mchezo wao wa ufunguzi katika dimba la Machakos Ijumaa Novemba 29.
Mara ya mwisho Rwanda kutwaa taji hilo ilikuwa ni mwaka 1999 na tangu wakati huo imepoteza katika fainali tano, mara tatu dhidi ya Uganda (2-0 mwaka 2003, 2009 kwa penati 3-2 na mwaka 2011 na mara moja dhidi ya Sudan mwaka 2007 pamoja na fainali ya mwaka 2005 dhidi ya Ethiopia mwaka 2005.
Full team:
Goalkeepers: Jean Claude Ndori, Jean Luc Ndayishimiye and Marcel Nzarora;
Defenders: Michel Rusheshangoga, Emery Bayisenge, Mwemere Ngirishuti,
Fitina Obalenga, Ismail Nshutinamagara, James Tubane and Abouba
Sibomana;
Midfielders: Jean Baptiste Mugiraneza, Mohamed Mushimiyimana, Haruna
Niyonzima ©, J. Claude Iranzi, Fabrice Twagizimana and Andrew Buteera;
Strikers: Meddie Kagere, Jacques Tuyisenge, Hussein Cyiza Mugabo and Michel Ndahinduka.
No comments:
Post a Comment