Ngorongoro Heroes |
Rwanda U-20 |
Timu ya
Taifa ya Rwanda ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 imewasili jijini Dar
es Salaam hii leo kwa ndege ya RwandAir kwa ajili ya
mechi mbili za kirafiki dhidi ya Ngorongoro Heroes.
Rwanda yenye
msafara wa watu 27 wakiwemo wachezaji 20 itafikia hoteli ya Sapphire. Mechi
hizo zitachezwa Julai 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa Chamazi na Julai 16 mwaka
huu Uwanja wa Taifa.
Ngorongoro
Heroes tayari iko kambini chini ya Kocha Jakob Michelsen na msaidizi wake Adolf
Rishard kujiwinda kwa mechi hizo ambazo ni sehemu ya maandalizi ya kuivaa
Nigeria.
Mechi dhidi
ya Nigeria ambayo ni ya kwanza ya raundi ya pili kusaka tiketi ya kucheza
fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Algeria itachezwa Julai 29
mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment