Mwanza
imejipatia tiketi ya kucheza fainali ya michuano ya Copa Coca-Cola 2012 baada
ya leo asubuhi (Julai 13 mwaka huu) kuilaza Temeke mabao 3-1 katika mchezo
uliofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Hadi dakika
90 za kawaida zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1. Mwanza
walitangulia kufunga dakika ya tatu kupitia kwa Jamal Mtegeta kabla ya Temeke
kusawazisha kwa penalti dakika ya 56 iliyowekwa wavuni na Baraka Ntalukundo.
Mabao
mengine ya Mwanza yaliyoipatia tiketi ya kucheza fainali keshokutwa (Jumapili)
yalifunga katika dakika 30 za nyongeza. Mtegeta alitikisa wazu dakika ya 94
kabla ya Dickson Ambundo kukwamisha la tatu dakika ya 108.
Nusu fainali
ya pili itachezwa leo jioni ikikutanisha timu za Morogoro ambayo kwenye robo
fainali iliibamiza Mara mabao 4-0 na Tanga iliyopata ushindi wa bao 1-0 dhidi
ya Dodoma.
No comments:
Post a Comment