Taslima law
chambers advocate imemwandikia barua katibu mkuu wa yanga ikitaka mkutano wa
uchaguzi uhairishwe kwasababu ni batili kwa kuwa katiba halali ya yanga ni ile
ya mwaka 1968 na si nyingine.
Barua
imesema kuna wanachama wa kadi ya katiba ya mwaka 1968 watakosa haki yao ya kikatiba
ya kushirikia uchaguzi kwasababu majina yao hayajaorodheshwa katika orodha
baada ya katiba ya sasa kutengenezwa .
Barua hiyo imetoa
rai kuwa uchaguzi huo uhairishwe ili kuepusha matatizo ya kisheria yanayo weza
kutokea na kunyima kutoa nafasi kulitatua suala hilo.
Barua hiyo
imesainiwa na na Taslima wakili wa Taslima
Law Chambers na nakala mbalimbali kusambazwa kwa mwenyekiti wa DRFA ,
msajili wa vyama vya michezo na katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF.
Barua hiyo
imesema usajili wa wadhamini ambao ni trusteeship
kama Yanga unafanyika kisheria chini ya sheria ya the Trustees incorporation
Act (cap318R.200) na si vinginevyo .
Ofisi ya
mrajisi mkuu tayari imeshaelekeza kimaandishi kuwa wanatambua wadhamini
waliotokana na katiba ya mwaka 1968 tu.
Kuna uamuzi
wa mahakama ya hakimu mkazi kisutu ya tarehe 1/07/2010 kwenye shauri la madai
no 98 la 2010 unaelekeza kuwa uchaguzi wowote utafanyika Yanga uzingatie katiba
ya mwaka 1968 hivyo uchaguzi wowote utafanyika bila kuzingatia katiba hiyo ni
batili
No comments:
Post a Comment