Mgombea wa
nafasi ya mwenyekiti katika uchaguzi mdogo wa klabu ya Yanga Yusufu Manji
amefanya kampeni yake ya kwanza jioni hii akiwa na wagombea wengine wa nafasi
za makamu mwenyekiti na ujumbe walio katika kambi moja Abdalah Bin Kleb, Clement
Sanga na Musa Katabalo, George Manyama na Lameck Nyambaya katika mkutano wa
kampeni uliofanyika katika uwanja wa Kaunda makao makuu ya klabu hiyo
Manji akiwa na
wapambe wake na wazee wa baraza la wazee wakiongozwa na mzee Ibrahim Akilimali
wamewataka wanachama kuwachagua wao ili kuweza kuwaongoza katika kipindi cha
miaka miwili ya awamu hii ya uongozi iliyosalia ili kuwaletea maendeleo
wanayanga.
Manji ambaye
si muongeaji sana alifika katika mkutano huo saa 11 jioni na kuwataka wanachama
waliokuwa wakimsikiliza kumchagulia viongozi wenzake watakao unda kamati ya
utendaji itakayo kuwa ikifanya kazi kwa vitendo na si maneno.
Amewataja
wagombea anaowataka katika safu yake kuwa ni Abdalah Bin Kleb, Musa Katabalo, Clement
Sanga na George Manyama ambao anaamini wataunda kamati yenye nguvu na ya maendeleo.
Awali akimtambulisha
kwa wanachama waliokusanyika katika uwanja wa makao makuu ya klabu hiyo
yaliyoko katika makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani katibu wa baraza la
wazee Ibrahim Akilimali amesema ni wagombea hao ndio waliompa jeuri ya kusema
anazo shilingi milioni 750 kwa lengo kuuondosha na kuubomoa uongozi uliopita
chini ya aliyekuwa kwenyekiti wakati huo Loyd Nchunga.
Akilimali
amesema katika zoezi la kuomba kura wagombea hao hawatapata nafasi ya
kutembelea matawi yote hivyo basi matawi ambayo yatapata nafasi ya kutembelewa
na wagombea hao ni Makangarawe ,Kigamboni
na Kawe.
Akilimali
amewataka wagombea wamuunge mkono Yusufu Manji na wagombea wengine wa safu
ambayo ameipendekeza yeye Manji ili waweze kuleta maendelea ndani ya klabu hiyo.
Kwa upande
wake Abdalah Bin Kleb mgombea wa nafasi ya ujumbe amewataka radhi wanachama
huko katika matawi kwa kushindwa kutokea kwenye kampeni kwasababu alikuwa bize
na usajili lakini amesema akipata uongozi atapita matawini kwa ajili ya
kuwashukuru.
Manji pia
amesema anajua wanaingia kwenye uchaguzi huku wakiwa na deni la mabao matano
waliyofungwa na wapinzani wao wa jadi Simba na kwamba deni hilo litalipwa
watakapo kuwa katika uongozi.
Pia amesema hataweza kusema sera zake kwa kuwa
wanachama wanajua ni nini wanataka lakini atafanya kwa vitendo na si maneno
huku akitumia maneno nipeni vitendea kazi nifanye kazi
No comments:
Post a Comment