![]() |
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la pili la Said Bahanuzi Mbuyu Twite akiwa kati. |
![]() |
Mbuyu Twite akiwa na Simion Msuva wakishangilia bao la kwanza la kujifunga Coast |
![]() |
Mbuyu Twite akipiga krosi kuelekea lango la Coast Union kupiga nyuma ni Nsa Job. |
Mabingwa wa kombe la kagame Yanga hii leo imeilaza timu ngumu ya Coast Union ya Tanga kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Coast ndio waliokuwa wa kwanza kuandika bao mapema kipindi cha kwanza likifungwa na kiungo wake Razak Khalfani kwa shuti lililomshinda mlinda mlango wa Yanga Ally Mustafa'Bartez'.
Mabao ya Yanga yalipatikana katika kipindi cha pili, la kwanza likitokana na mpira wa kujifunga kwa kichwa na mlinzi Philipo huku bao la pili likifungwa na Said Bahanuzi kwa shuti lililogonga mwamba na kisha kutinga wavuni.
Coast walilazimika kucheza pungufu katika sehemu kubwa ya kipindi cha pili cha mchezo kufuatia kiungo wake Jeri Santo kutolewa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu baada ya kutoa lugha chafu kwa mwamuzi.
No comments:
Post a Comment