KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, November 25, 2012

BAADA YA USHINDI WA BAO 2-0 DHIDI YA SUDAN KOCHA KIM POULSEN NA NYODO ZAKE:“hatukuweza kutengeneza nafasi zaidi lakini pia hatukuwapa na wao nafasi nyingi. Ilikuwa ni chipukizi na tumecheza vizuri.”


Simon Msuva akiwaburuza walinzi wa Sudani.

Mabao mawili ya kipindi cha kwanza yaliyofungwa na John Raphael Bocco yameiwezesha timu ya taifa ya Tanzania Bara ‘The Kilimanjaro stars’ kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sudini mchezo ambao ulikuwa ni wa pili wa kundi la B wa michuano ya kombe la Chalenji mchezo ambo umefanyika katika uwanja wa Namboole. 

Katika mchezo huo ambao ulikuwa ukichezeshwa na mwamuzi raia wa Uganda Dennis Batte, Kilimanjaro Stars ilipigana vema katika kipindi cha kwanza ambapo kiungo wa pembeni Mrisho Ngasa alionekana kuwasumbua walinzi wa Sudani huku akisaidiana na Simon Nsuva na John Bocco.

Mabao yote mawili yalipatikana kutokana na jitihada za Ngasa kuwatoka walinzi wa Sudani na kupenyeza pasi kwa Bocco ambaye mara zote alitumia vizuri kasi ya Ngasa kuwatoka walinzi na kutumbukiza mpira wavuni.

Kipindi cha pili Sudan walirejea na nguvu mpya wakijaribu kuunganisha timu yao vema na kuwanyima nafasi washambuliaji wa Kilimanjaro Stars kupata mipira mingi.

Sudani maarufu kama mamba wa mto Nile walikuwa wakiwatumia washambuliaji wao Sadam Abutalib na Hamoda Bashir ambao hata hivyo walishindwa kutumbukiza mipira wavuni.

Baada ya mchezo kocha wa Kilimanjaro Stars Kim Poulsen amekaririwa akisema
“tunapaswa kubadilisha mfumo wa uchezaji wetu. Tumetumia wachezaji wetu vijana na tulichokuwa tunakitafuta ni kidhamu ya kimchezo ya timu. Tumewafunga na hatukuwapa nafasi wapinzani kupata bao”.

“hatukuweza kutengeneza nafasi zaidi lakini pia hatukuwapa na wao nafasi nyingi. Ilikuwa ni chipukizi na tumecheza vizuri.”
Sam Ssimbwa kaloweshwa na Warundi.
 Katika mchezo wa mapema hii leo kikosi cha kocha Sam Ssimbwa cha Somalia kimeanza vibaya baada ya kuchapwa mabao 5-1 na Burundi mchezo pia uliopigwa katika uwanja huohuo wa Namboole.

Mabao ya washindi yalifungwa na Chris Nduwagira, Sulemani Ndikumana na Yusuf Ndikumana huku bao la Somalia maarufu kama Nyota wa bahari likifungwa na Mohammad Jabril kwa njia ya mkwaju wa penati.

Ushindi wa Burundi wa mabao mengi umewaweka katika uongozi wa kundi hilo la B kwa tofauti ya mabao kufunga na kufungwa dhidi ya Kilimanjaro Stars
 Kesho ni zamu ya kundi C ambapo katika mchezo wa kwanza timu Zanzibar watakuwa wakicheza dhidi ya Eritrea na katika mchezo wa pili Malawi watakuwa wakikumbana dhidi ya Rwanda.

No comments:

Post a Comment