Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeteua waamuzi kutoka Angola
kuchezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa
Stars) na Morocco (Lions of the Atlas).
Mechi
hiyo ya kundi C itachezwa Machi 24 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam. Ivory Coast ndiyo inayoongoza kundi hilo ikiwa na pointi
nne na kufuatiwa na Taifa Stars yenye pointi tatu.
Mwamuzi
wa mechi hiyo ni Helder Martins de Carvalho wakati mwamuzi msaidizi
namba moja ni Inacio Manuel Candido huku Ricardo Daniel Cachicumi akiwa
mwamuzi msaidizi namba mbili. Mwamuzi wa mezani (fourth official) ni
Antonio Muachihuissa Caxala.
Waamuzi
hao watawasili nchini saa 1.20 usiku Machi 22 mwaka huu kwa ndege ya
Kenya Airways wakitokea Luanda, Angola kupitia Nairobi, Kenya.
Kamishna
wa mechi hiyo atakuwa David Fani kutoka Botswana anatarajiwa kuwasili
Machi 22 mwaka huu saa 1.45 usiku kwa ndege ya South African Airways.
Naye
mtathmini wa waamuzi (referee assessor) Neermal Boodhoo kutoka Afrika
Kusini atawasili nchini Machi 22 mwaka huu 1.45 usiku kwa ndege ya South
African Airways.
No comments:
Post a Comment