Mshambuliaji wa Yanga Hamis Kiiza akijaribu kumtoka beki wa Ruvu shooting |
MSHAMBUJIA
Hamisi Kiiza leo ameiwezesha Yanga kuondoka na pointi tatu baada ya kuilaza 1-0
Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga sasa imefikisha pointi 48 baada ya kucheza mechi 21, ikiizidi Azam FC kwa
pointi 11 iliyo katika nafasi ya pili, ingawa ina mchezo mmoja huku Simba ikiendelea
kushika nafasi ya tatu kwa pointi 34.
Kikosi cha Yanga ni; Ally Mustafa ‘Barthez’,
Juma Abdul, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Athumani Iddi
‘Chuji’, Simon Msuva, Frank Domayo, Hamisi Kiiza, Nizar Khalfan na Haruna
Niyonzima.
Kikosi cha Ruvu Shooting; Benjamin Haule, Michael Aidan, Mau Bofu, Ibrahim
Shaaban, Mangasini Mbonosi, Gedion Tepo, Ayoub Kitala, Ernest Ernest, Hassan
Dilunga, Said Dilunga na Abrahman Mussa.
(Source Lenzi ya michezo blog)
No comments:
Post a Comment