SIMBA SPORTS CLUB SIMBA
P.O.BOX
15318 | TEL+255 222183330 |FAX +255 222183330
|MSIMBAZI/MCHIKICHI STREET | DAR ES SALAAM | TANZANIA | EMAIL simbasportsclub@yahoo.com|WEBSITE www.simba.co.tz| AFFILIATED TO TFF, DRFA and IDFA
16/03/2013
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu
wana habari,
KUMEKUWAPO
na taarifa za kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Simba uliopangwa
kufanyika Kesho (Machi 17, 2013) jijini Dar
es Salaam kujadili mustakabali wa klabu.
Ikumbukwe
kwamba Mkutano Mkuu wa Wanachama ndiyo chombo cha juu kabisa cha maamuzi kwa
klabu yetu. Katiba ya Simba
SC imeupa Mkutano Mkuu hadhi ya
juu mno na ndiyo maana imeweka utaratibu wa kufanyika kwake.
Miongoni
mwa utaratibu ni kwamba ni lazima uitishwe na Mwenyekiti aliye madarakani wa
klabu. Kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji, ndiye atakayepanga ajenda,
mahali na wakati wa kufanyika kwa mkutano wenyewe.
Katika
miaka ya nyuma, zilikuwepo nyakati ambapo klabu ilikaa hadi miaka mitatu pasipo
kuitishwa kwa Mkutano Mkuu wowote wa wanachama. Hakuna mwanachama au kikundi
chochote kilichojitokeza kudai mkutano wa dharura wakati huo ingawa ilikuwa
ikifahamika kwamba huo ulikuwa ni ukiukwaji mkubwa wa katiba ya klabu.
Tangu
uongozi huu uingie madarakani takribani miaka mitatu iliyopita, mikutano mikuu
miwili ya wanachama imefanyika kwa mujibu wa KATIBA. Mungu akijaalia, uongozi
huu utafanya mkutano mwingine wa kawaida wa wanachama baadaye mwaka huu.
Hata
hivyo, kwa kuzingatia hali halisi ya klabu, Mwenyekiti wa Simba, Alhaji Ismail
Aden Rage (Mb), mwezi uliopita alitangaza dhamira yake ya kuitisha Mkutano Mkuu
wa Dharura wakati wowote kuanzia sasa.
Rage
alisema mkutano huo ungekuwa na ajenda moja tu; Kujadili Mwenendo wa Klabu
kwenye mashindano inayoshiriki msimu huu.
Kwa
bahati mbaya, Mwenyekiti alishikwa na maradhi na akapelekwa India kwa
matibabu na yuko huko hadi Mola atakapomjalia afya njema na kurejea. Kuna
uwezekano mkubwa, Inshallah, akarejea mwishoni mwa wiki ijayo.
Hii
maana yake ni kwamba uongozi umeridhia kufanyika kwa Mkutano wa wanachama.
Kimsingi, kama uongozi umeridhia, hakuna
mwanachama mwingine anayeweza kuitisha mkutano mkuu mwingine.
Mwenyekiti
ameruhusiwa kuitisha Mkutano Mkuu kwa sababu alichaguliwa na wanachama na hivyo
ana nguvu ya kisheria (locus standi) kufanya
hivyo. Hawa wengine wanaoitisha mkutano wana nguvu gani ya kisheria kufanya
hivyo? Walichaguliwa na nani kuwakilisha wanachama? Lini na wapi?
Uongozi
pia unaweza kuitisha mkutano kwa vile wenyewe ndiyo wenye leja ya wanachama.
Klabu sasa ina database yake ya kompyuta inayotambua wanachama walio hai na
wasio hai.
Kwa
kutumia database hiyo, uongozi huu unatambua wanachama walio hai na wasio hai. Hakuna
mtu mwingine yeyote, aliye nje ya uongozi huu anayefahamu wanachama walio hai
na wasio hai. Hao wanachama wanaoitana kufanya mkutano, wamehakikiwa na nani
kubaini uhalali wao huo?
Uongozi
wa Simba SC
unaona kwamba wale wanaolazimisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wana ajenda
binafsi na si za maslahi ya klabu. Kama kweli
wangekuwa na nia njema na klabu wangesubiri mkutano ambao utaitishwa punde.
Kwani,
kuna uharaka gani wa kufanyika mkutano kesho? Kwanini hawataki Mwenyekiti,
ambaye wanachama walimpa mamlaka ya kuongoza klabu kwa kipindi cha miaka minne,
awepo kwenye mkutano huo?
Kwanini
hawataki kuungana na wana Simba wengine kumwombea Mwenyekiti kwa Mungu ili
amwepushe na ugonjwa na kumrejesha salama hapa nyumbani? Kwanini mikutano hii
iitishwe katika kipindi ambacho uongozi umefungua mikono yake na kukaribisha
kila mmoja mwenye mapenzi mema na klabu kuja kuchangia?
Kwenye
macho ya Katiba ya Simba na sheria za Tanzania, huu mkutano wa kesho ni
batili na una lengo la kuleta vurugu na mifarakano kwenye jamii na michezo kwa
ujumla wake. Michezo ni amani na furaha na michezo si vurugu.
Tayari
uongozi wa Simba umetoa taarifa kwa Jeshi la Polisi na Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) kuhusiana na ubatili wa mkutano huo. Tunapenda kuwaomba
wanachama wetu wasiopenda fujo na vurugu kwenye michezo kukaa mbali na mkutano
huo kwa vile vyombo vya dola vitaufuatilia.
Uongozi
hautajiingiza katika kutoa dhamana au msaada wa namna yoyote kwa yeyote ambaye
atachukuliwa hatua na vyombo vya dola kutokana na kujihusisha na mkutano huo.
Pia,
Simba SC
inatoa wito kwa vyombo vya habari kuwa makini wakati vinaporipoti matukio ya
vurugu kwenye michezo. Kabla mtu hajahojiwa kujieleza kama
mwanachama wa Simba, ni vema kwanza akaonyesha kadi yake ya uanachama na risiti
za malipo yake.
Wakati
mwingine, waandishi huwa tunawapa nafasi kwenye vyombo vyetu vya habari watu
ambao hawana mchango wowote kwenye kukuza michezo bali kuleta vurugu. Kwanini,
tungejiuliza, ni watu wale wale ambao kila mwaka huonekana wakati wa vurugu na
wakati wa amani huwa hawaonekani?
Kwanini,
vyombo vyetu vinatoa nafasi kwa watu ambao lengo lao ni kuhakikisha vilabu
vyetu vinazidi kubaki nyuma, vinakuwa na vurugu kila wakati na michezo
inaonekana kama ni sehemu ya wahuni na watu wasio na utaratibu?
Mpira
bado haujaleta tija kubwa kwenye uchumi wa Tanzania
na kunufaisha wachezaji kwa sababu baadhi ya watu makini na makampuni makubwa
yanaogopa kujiingiza kwenye michezo kwa sababu ya tabia kama
hizi.
Ni
vema vyombo vya habari vikafanya jitihada kubwa katika kuwatambua waleta
vurugu, si katika klabu ya Simba pekee, bali kwenye sekta ya michezo kwa
ujumla, ili visiwape nafasi ya kuharibu na badala yake vitoe nafasi kwa wale
wenye lengo la kujenga.
Tunasisitiza,
uongozi huu utaitisha Mkutano Mkuu wa Wanachama Wote mara baada ya kurejea kwa
Mwenyekiti.
Imetolewa
na
Ezekiel
Kamwaga
Ofisa
Habari
Simba
SC
No comments:
Post a Comment