Taifa
Stars imeanza kambi jana jioni (Machi 16 mwaka huu) ambapo wachezaji 14
kati ya 23 walioitwa wameripoti na kufanya mazoezi leo asubuhi chini ya
Kocha Kim Poulsen.
Wachezaji
walioripoti ni nahodha Juma Kaseja kutoka Simba na msaidizi wake Aggrey
Morris wa Azam, Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir
Haroub (Yanga), Nassoro Masoud Cholo (Simba), Shomari Kapombe (Simba) na
Salum Abubakar (Azam).
Wengine
ni Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Frank Domayo (Yanga),
Mwinyi Kazimoto (Simba), Mrisho Ngasa (Simba) na Simon Msuva (Yanga).
Wachezaji
Hussein Shariff, Issa Rashid na Shabani Nditi ambao timu yao ya Mtibwa
Sugar jana ilicheza mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) mjini Turiani
wataripoti kambini leo jioni.
Kikosi
hicho kitakamilika Jumanne asubuhi baada ya wachezaji walio katika
kikosi cha Azam nchini Liberia kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho
kurejea nchini. Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe
ya Jamhuri ya Kidemorasi ya Congo (DRC) wanatarajiwa kutua nchini kesho
usiku.
No comments:
Post a Comment