Nyota namba moja katika mchezo wa tenisi nchini Uingereza Andy Murray amefanikiwa kushinda pambano lake dhidi ya Richard Gasquet na kupata ushindi wa seti 6-7 (3/7), 6-1, 6-2,
na kufanikiwa kuingia fainali ya michuano ya Sony Open ambapo atapambana na David Ferrer.
Gasquet ambaye ni namba nane kwa ubora alianza mchezo huo vema na kutawala katika seti ya kwanza ambalo alifanikiwa kupata tie-break, lakini hata hivyo Murray alirejea na kuchukua hatamu ya mchezo katika seti ya pili na ya tatu ya pambano ambalo lilikuwa zuri na la kupendeza la nusu fainali.
Wiki ijayo Murray
atakuwa akipambana na Ferrer ambaye alimchapa mkongwe kutoka nchini Ujerumani Tommy Haas
katika nusu fainali ya kwanza.
Endapo Murray atafanikiwa kushinda pambano hilo basi litampandisha juu kiubora zaidi ya mpinzani wake mkubwaRoger
Federer.
No comments:
Post a Comment