Mwanariadha wa kenya mwenye mbwembwe Ezekiel Kemboi
ametangaza mpango wake wa kustaafu baada ya michezo ya Olimpiki ya mwaka
wa 2016 mjini Rio de Janeiro huko Brazil .
Kemboi anayesifika kwa mbio za kuruka maji na
viunzi analenga kushinda medali ya Dhahabu kwa mara ya tatu katika mbio
za Olimpiki.
"Nimeiwakilisha Kenya kwa muda wa miaka 13
mtawalia, nitakamilisha maisha yangu kama mkimbiaji baada ya Rio 2016"
Kemboi alidokeza katika hafla ya zawadi mjini Eldoret eneo la Bonde la
ufa.
Mwanariadha huyo mshindi mara mbili wa Olimpiki
na mara tatu duniani atajitosa katika mchezo wa Golf atakapostaafu.
Mchezo huo utajumuishwa kama mchezo wa Olimpiki mwaka 2016.
Kemboi mwenye umri wa miaka 31 alimshinda
Conseslus Kipruto ili kupata taji lake la tatu la mkimbiaji bora duniani
wa kuruka maji na viunzi kwa wanaume mjini Moscow mwezi uliopita
No comments:
Post a Comment