Kocha wa timu ya taifa ya Nigeria Stephen Keshi amesema hataidharau timu ya taifa ya Ethiopia
wakati watakapo kutana katika mchezo wa hatua ya mtoano kuelekea kufuzu kupata nafasi ya kucheza kombe la dunia.
Ethiopia ndio inayoonekana kuwa kibonde kuelekea katika mzunguko huo wa mwisho wa safari ya kuwasili nchini Brazil.
Amenukuliwa akisema
"Hawakufika katika hatua hii kwa bahati mbaya, na hiyo inatueleza mengi juu ya ukweli kwamba Ethiopia ni timu.
"Ethiopia ina aina yake ya uchezaji isiyotabirika ambayo inafanya kuwa hawaeleweki kwa wapinzani wao. Tunakwenda kucheza michezo yote kama fainali"
Timu hizo mbili zilikutana katika michezo ya mataifa ya Afrika hatua ya makundi mjini Rustenburg mwezi Januari, mchezo ambao Super
Eagles ilishinda kwa mabao 2-0 mchezo ambao ulikuwa ni njia ya Nigeria kutawazwa taji la Afrika.
Super Eagles imekuwa ikicheza michezo yake katika mji wa Calabar
tangu 2012, lakini sasa watakuwa wakielekea katika uwanja wa taifa wa Abuja kwa ajili ya michezo yote miwili.
No comments:
Post a Comment