Aliyekuwa nahodha wa timu ya soka ya Uholanzi, Ruud
Krol ametia saini mkataba wa miezi miwili kuwa kocha wa timu ya Tunisia
katika michuano ya kufuzu kombe la Dunia barani Afrika.
Carthage Eagles watacheza na Cameroon kwa ligi
mbili mwezi Octoba na Novemba ambapo mshindi atapata nafasi ya kucheza
katika fainali za mwaka ujao nchini Brazil.
Krol pia atasalia kuwa kocha wa timu ya CS Sfaxien ,klabu ambayo alisimamia katika michuano ya Tunisia mwezi Mei.
Sfaxien pia wamefuzu kishiriki nusu fainali ya kombe la shirikisho.
Shirikisho la soka la Tunisia limemchagua Krol
kuchukua nafasi ya Nabil Maaloul ambaye alijiuzulu baada ya timu hiyo
kupoteza mechi ya finali ya makundi kwa mabao 2-0 didhi ya Cape Verde
tarehe 7 Septemba.
Wakati huo huo matokeo hayo yalimaanisha kuwa
Tunisia haikufuzu kushiriki katika fainali za makundi lakini baadaye
walipata afueni wakati ilipobainika kuwa Cape Verde walishirikisha
mchezaji asiyestahili wakati wa mechi hiyo.
Haya yalifuatiwa na shirikisho la soka duniani
kutuza Tunisia ushindi wa mabao 3-0,na kuwaruhusu kuendelea katika
fainali ya michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia barani Afrika
No comments:
Post a Comment