Na Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Mradi
wa Football for Hope kusaidia watoto na wasiojiweza kupitia mpira wa
miguu uliofadhiliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)
mkoani Iringa utafunguliwa rasmi Oktoba 13 mwaka huu.
FIFA
hutoa mradi huo kwa baadhi ya nchi kwa kuzingatia mambo mbalimbali
ikiwemo utawala bora, lakini kwa kupitia taasisi zisizo za kiserikali
(NGOs) ambapo kwa Tanzania umepatikana kupitia taasisi ya Iringa
Development of Youth, Disabled and Child Care (IDYDCC).
Rais
wa TFF, Leodegar Tenga ameishukuru FIFA kwa msaada huo, kwani ni mkubwa
na kuongeza kuwa ni matumaini yake utatumika kwa lengo lililopangwa.
Amesema
mradi huo wa FIFA ambao ni wa kusaidia watoto kielimu na wasiojiweza
kwa kupitia mpira wa miguu haukupita moja kwa moja TFF ni mzuri kwani
moja ya mambo uliofanikisha ni kuwepo jengo na sehemu ya watoto kucheza.
Ni
wastani wa nchi kumi tu duniani kwa mwaka zinapata mradi huo kutoka
FIFA, jambo ambalo Rais Tenga amesema linachangiwa pia na uhusiano na
ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na shirikisho hilo.
KAMATI YA WANAWAKE, TWFA YAPONGEZWA
Kamati
ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) na Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA)
wamepongezwa kwa kuhakikisha akina mama wanacheza mashindano mbalimbali.
Pongezi
hizo zimetolewa na Rais wa TFF, Leodegar Tenga ambapo amesema timu za
wanawake zimekuwa zikishiriki katika mashindano mbalimbali licha ya
ukweli kuwa hadi sasa hakuna udhamini kwenye mchezo huo.
Amesema
mpira wa miguu unaendeshwa na udhamini na kuchangia, jambo ambalo
linafanikishwa kwa kiasi kikubwa na uwazi katika matumizi ya fedha,
jambo ambalo hivi sasa lipo ndani ya TFF.
Rais
Tenga amesema baada ya kuanzisha Kamati ya Ligi, hivi sasa TFF inapata
asilimia 4.5 tu ya mapato ya mechi za ligi kutoka asilimia 33 iliyokuwa
ikipata wakati anaingia madarakani mwaka 2004.
Amesema
asilimia hiyo 4.5 haiwezi kuendesha mpira na ndiyo maana nguvu
zinaelekezwa katika kutafuta wadhamini na kuchangia. Pia TFF inatoa
zaidi ya asilimia 15 ya Fedha za Msaada wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu
(FAP) kutoka FIFA kwenye mpira wa miguu wa wanawake ambapo ni nchi
chache zinazofikia kiwango hicho.
Hivyo,
ametoa mwito kwa kampuni kujitokeza kudhamini au kuchangia timu za
Taifa za mpira wa miguu za wanawake ambazo zinashiriki mashindano
mbalimbali mwaka huu, kwani gharama za kuziendesha ni kubwa.
Timu
ya wakubwa (Twiga Stars) inacheza mashindano ya mchujo ya Fainali za
Afrika (AWC) zitakazofanyika mwakani nchini Namibia wakati ile ya chini
ya miaka 20 inacheza mashindano ya Dunia ambayo fainali pia zitachezwa
mwakani nchini Canada.
MECHI YA YANGA, MTIBWA YAINGIZA MIL 97/-
Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) iliyochezwa jana (Oktoba 6 mwaka huu)
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Yanga na Mtibwa Sugar imeingiza
sh. 97,557,000.
Watazamaji
waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo namba 46 lililochezeshwa na
Isihaka Shirikisho kutoka Tanga walikuwa 17,313. Yanga ilishinda mabao
2-0.
Viingilio
katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh.
20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 23,453,748.95 wakati Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 14,881,576.27.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 11,925,635.06,
gharama ya kuchapa tiketi ni sh. 3,171,190 wakati gharama za mchezo ni
sh. 7,155,381.04.
Kamati
ya Ligi sh. 7,155,381.04, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF)
sh. 3,577,690.52 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA) sh. 2,782,648.18.
No comments:
Post a Comment