KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, October 7, 2013

MVUTA SIGARA WILSHERE AKIRI KOSA NA KUAHIDI KUACHA TABIA HIYO

Baada ya bosi wa washika mitutu wa jiji la London Arsene Wenger kumuonya kiungo wake Jack Wilshere ambaye alikataa katakata juu ya mwenendo wake wa hovyo wa kuvuta sigara mbele ya hadhira, hatimaye kiungo huyo amekubali kosa na kuahidi kuwa haitatokea tena.
Wilshere amesema kuwa alifanya kosa baada ya kupigwa picha akivuta sigara nje ya ukumbi mmoja wa starehe za usiku
'nightclub' jijini London.

Bosi wa Wenger aliweka hilo wazi Ijumaa iliyopita ambapo alikaririwa akisema hakubaliani hata kidogo na tabia hiyo na licha ya awali kiungo huyo wa kimataifa wa England kukanusha, sasa amekubali kufanya kuhukumiwa kwa kosa hilo.

Akiongea na mtandao wa klabu hiyo Wilshere amenukuliwa akisema 
"I made a mistake,"
"Players make mistakes. I'm not a smoker.

"Nimeongea na bosi na kunitaka kueleza kilichotokea na nimemueleza na hatimaye kutatua hilo na kunirejesha kikosini na nina matumaini na kumjibu kwa kufunga goli dhidi ya West Brom.

"Haitatokea tena, mimi si mvuta sigara hivyo nadhani hiyo itakuwa ni mara ya mwisho."

No comments:

Post a Comment