Afisa wa Match Hospitality akamatwa Brazil |
Maafisa wa polisi nchini Brazil wamemkamata afisa
mkuu mtendaji wa kampuni mshirika wa FIFA kwa tuhuma za uuzaji tiketi za
kombe la dunia kinyume na kanuni.
Ray Whelan ambaye ni meneja mkuu mtendaji wa
kampuni mshirika wa FIFA Match Hospitality alikamatwa katika hoteli moja
huko Rio de Janeiro , inayotumika pia na maafisa wa shirikisho la FIFA.
Juma lililopita watu wengine 11 walikamatwa kwa kuuza tiketi za kombe la dunia kinyume na kanuni za FIFA .
Polisi walisema kuwa kikundi hicho kilikuwa
sehemu ya genge kubwa la kimataifa ambalo lilikuwa likiuza tiketi ambazo
zilikuwa zimetengewa makundi maaluma ikiwemo tiketi zilizokuwa
zimetengewa wachezaji .
Polisi nchini Brazil walisema kuwa tayari genge
hilo lilikuwa limetia kibindoni takriban dola milioni 90 katika mauzo
hayo ambayo yamekuwa yakiendelea katika mashindano manne ya kombe la
dunia .
Kufuatia kashfa hiyo uchunguzi unaendelea
kubaini iwapo baadhi ya tiketi hizo zimeuziwa watalii ambao hawakujua
walikuwa wanakiuka sheria za shirikisho la soka duniani FIFA.
Kompyuta na vifaa vyengine vya kielektroniki
vilikamatwa na polisi kwa uchunguzi zaidi kutopka kwa mkahawa huo wa
kifahari ulioko Copa Cabana Palace Hotel
Kampuni hiyo ya Match Hospitality yenye makao yake huko Switzerland hadi sasa haijatoa taarifa zozote kufuatia ugunduzi huo.
Afisa anayeongoza uchunguzi huo Fabio Barucke,
amesema kuwa afisa huyo alikuwa na hati zinazomruhusu kuingia katika
afisi zote za fifa kwa hivyo alikuwa na uwezo wa kuzipata tiketi hizo.
Uchunguzi unaendelea.
No comments:
Post a Comment