KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, July 7, 2012

OLYMPIC LONDON:Wanamichezo wa Tanzania kuondoka kesho.


Wachezaji wa Tanzania wa Olympic
Jumla ya wanamichezo sita wa Tanzania waliofuzu vigezo vya kushiriki michezo ya mwaka huu ya Olympic wameagwa rasmi hapo jana katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa HYYAT REGENCE zamani Kempisk katikati ya jijini la Dar es salaam.
Viongozi mbalimbali wa vyama vya michezo walihudhuria HAFLA hiyo iliyokuwa ikiongozwa na mgeni rasmi naibu waziri wa habari michezo na utamaduni Amos Makala, viongozi mbalimbali wa kamati ya Olympic Tanzania na wanamichezo wenyewe ambao wanatarajiwa kuondoka nchini hapo kesho kuelekea jijini London kushiriki michezo hiyo
Waziri makala katika hotuba yake amewataka wanamichezo hao kujiamini na kujituma huku wakijua kuwa mamilioni ya watanzania wako nyuma yao na wanasuburi medali zao kwa hamu kubwa.
Amesema anaamini wamepata maandalizi ya kutosha chini ya kamati ya Olympic.
Lakini pia waziri makala alitumia fursa hiyo kuwataka wadau wajitokeze kudhamini na kufadhili michezo nchini huku akiwapongeza kampuni ya coca kola ambayo imedhamini safari kwa wanamichezo hao ambao kesho watakuwa wakiandamana na vikongozi wao.
   Wakati TOC ikisema itatoa shilingi milioni kumi  kwa atakaye fanya vizuri huku waziri wa zamani wa michezo wa zamani Mrisho Sarakikya katika kujaribu kuwapa hamasa zaidi amesema yuko tayari kutoa dola elfu mbili kwa yeyeto aatakayerudi nyumbani na medali.
Wachezaji watakao ondoka kesho ni pamoja na Msenduki Mohamed,Samsoni Ramadhani ambaye atakuwa nahodha,Mgdalena Mushi, selemani Kidunda Zakaria Mrisho na Faustine Musa.

No comments:

Post a Comment