Ramadel Falcao |
Mshambuliaji
wa Atletico Madrid Radamel Falcao amedai kuwa ana weza kuwashinda washambuliaji
wawili wakali katika ligi kuu ya nchini Hispania Lionel Messi na Cristiano
Ronaldo na kuwa mfungaji bora wa ligi ya nchi hiyo La Liga msimu huu.
Falcao
ambaye alifikisha jumla ya mabao 24 msimu uliopita baada ya kucheza michezo 33 ya
ligi hiyo alikuwa pia kivutio kwa soka lake zuri na kuwa nyuma ya wafungaji Lionel
Messi wa Barcelona aliyefunga jumla ya mabao 50 na Cristiano Ronaldo wa Real
Madrid aliyefunga jumla ya mabao 46 na kuwa katika mbio za ufungaji bora nchini
Hispania maarufu kama Pichichi.
Katika hatua
nyingine mfumania nyavu huyo wa kimataifa wa Colombia amesema changamoto ya ubora
wa wafungaji hao hodari wa mabao duniani kuelekea msimu mpya wa 2012-13 haita
mfanya yeye kujiona kuwa yuko nyuma lakini pia si kazi rahisi.
amenukuliwaFalcao
akisema
"Idadi
yao kubwa ya mabao kama ilivyo kwao si kwamba haliwezekani kwangu "
"Ninachotaka
ni kusheherekea mzuri na mashabiki. Na kwa malengo yangu na timu kwa ujumla
naamini watafurahi. 'Pichichi'? kwanini isiwezekani ? ukiwa na moyo kila kitu
kinawezekana."
Falcao,ambaye
ambaye amesaini mkataba miezi 12 iliyopita kwa ada ya uhamisho wa euro milioni €40
akitokea katika klabu ya Porto ya Ureno ameitabiria timu yake itakuwa
ikifurahia kampeni ya mafanikio.
Atletico inaanza
msimu mpya jumatatu wakianza kwa kuifuata Levante.
No comments:
Post a Comment