Beki wa Manchester United Rio Ferdinand ametozwa faini ya pauni za
Uingereza 45,000 sawa na dola za kimarekani $71,000 na chama cha mpira
cha England baada ya kupatikana na hatia ya kutumia lugha mbovu kwa
beki wa Chelsea Ashley Cole.
Halmashauri huru imempata na hatia kwa
kumkashifu Cole akitumia lugha inayopdhalilisha ukoo na kabila la
mpinzani kwa msemo wa maneno 'Choc ice' kwa maana mtu mweusi nje na
ndani mzungu.
Ferdinand alikanusha kua sivyo hivyo ila ni kwamba maanake ni mtu feki, au mnafiki.
Matamshi yaliyopeperushwa kwa mtandao wa Twitter
yalitokea baada ya Ashley Cole kutoa ushahidi mahakamani dhidi ya mdogo
wake Rio aliyedai kua alitukanwa na John Terry. Terry hakupatikana na
hatia.
No comments:
Post a Comment