Kikosi kamili cha viongozi na wachezaji Yanga
ambacho kipo nchini Rwanda kesho kitakuwa na mazungumzo na Rais Paul Kagame wa nchi
hiyo.
Yanga ambayo iko katika program yake
ya mazoezi inataria kucheza michezo miwili ya kirafiki ijumaa ikianza na Police fc ya huko.
Akiongera na Rockersports makamu
mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga amesema wanataraji kucheza mchezo wa
kwanza wa kirafiki dhidi ya Polisi fc Ijumaa
kabla ya mchezo wao wa pili na wa mwisho dhidi ya Rayol sports jumapili na jumatatu
watakuwa wakirejea nyumbani Tanzania kuendelea na program yao ya mazoezi ya
kujiwinda na ligi ya Vodacom.
Mabingwa hao wa kombe la Kagame
linalodhaminiwa kila mwaka na Rais Kagame waliwasili jana nchini humo kwa mwaliko wa Rais Kagame lakini pia ni sehemu ya muendelezo wa program ya mazoezi ya wiki moja kwa
ajili ya maandalizi ya ligi kuu ya Vodacom iliyosogezwa mbele mpaka September 15.
Hapo kabla Yanga ilikuwa imejipanga
kucheza mchezo mwingine dhidi ya mabingwa wa ligi ya Rwanda “Primus league” APR
lakini mchezo huo umefutwa.
No comments:
Post a Comment