KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, August 19, 2012

MBUYI TWITE KESHO TAIFA YANGA VS AFRIKAN LYON



Klabu bingwa  Afrika mashariki na kati Dar Young Afrikans (Yanga ) kesho watakuwa wakishuka dimbani kucheza dhidhi ya timu Afrika Lyon mchezo wa kirafiki utakao pigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo umeandaliwa na Kampuni ya VANNEDRIC(T)LTD kwa lengo la kutoa burudani kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam mara baada ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani lakini pia ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya vikosi vya timu hizo ambazo zinashirikia ligi kuu ya Tanzania bara.

Mchezo huo umepangwa kuanza saa 10 kamili na kila timu imeahidi kushusha vikosi vyao kamili vilivyo sajiliwa msimu huu.

Itakumbukukwa Yanga mara baada ya kutwaa Kombe la Kagame bado haijashuka tena dimbani kucheza mchezo wowote mbali ya kucheza mchezo mmoja na kombaini ya Kijitonyama.

Hii itakuwa ni fursa nzuri kwa mashabiki wa timu hiyo kongwe hapa nchini kuwaona kwa mara nyingine tena wachezaji wao pamoja na mlinzi nyota aliyejiunga na Yanga msimu huu akitokea APR ya Rwanda Mbuyi Twite.

Kwa upande wao African Lyon ambayo kwasasa inanolewa na kocha wa kigeni raia wa Argentina Pablo Ignacio Velez itakuwa na inataka kutumia mchezo huo ili kusahihisha makosa ya wachezaji wao baada ya mafundisho ya muda mfupi toka kwa kocha huyo.

Viingilio ni 5000,7000,10000 na 15,000.

 

No comments:

Post a Comment