Klabu bingwa
barani Afrika Esperance ya Tunisia imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya
klabu bingwa Afrika baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya ndugu za wa
Etoile du Sahel.
Mchezo huo
umefanyika mbele ya mashabiki wa timu moja tu wa Etoile uliingiwa na vurugu
kubwa za kuvamia uwanja baada ya kila bao kiasi polisi kulazimika kutumia gesi
kutawanya watu kutoka katika uwanja.
Karim
Aouadhi alifunga bao la kwanza katika dakika ya 41 ilhali Yanick N'Djeng akifunga goli la pili
katika dakika ya 74 na kuamsha furaha toka kwamashabiki wao waliokuwa katika
jiji la Tunis,
Ushindi huo
ni muendelezo wa rikodi yao ya kutokufungwa katika jumla ya michezo 20 ndani ya
misimu miwili.
Katika michezo
mingine ya kundi A, AS Chlef imepoteza mchezo wake baada ya kufungwa kwa mabao 2-1na
wageni timu ya Sunshine Stars ya Nigeria mchezo uliopigwa ijumaa jioni matokeo
ambayo yanaifanya AS Cleif kushindwa kusonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali
ya klabu bingwa barani Afrika.
Sunshine iko
mbele ya Etoile kwa points tatu wakati ambapo Chlef yenyewe imepoteza michezo
yake yote minne ya hatua ya makundi mpaka sasa na imesalia mkiani katika kundi
hilo bila ya point.
Katika mchezo
huo Sunshine ilianza kupata bao mudamfupi kuelekea mapumziko kupitia kwa
mkameroon Medrano Tamen aliyemalizia mpira wa counter-attack kulekea katika klabu hiyo ya
nchini Nigeria.
Wenyeji walifanikiwa
kusawazisha muda mfupia baada ya mapumziko kupitia kwa mkameroon mwingine Anicet
Eyenga lakini matumaini ya Chlef kushinda yalimalizwa na Sabri Gharbi alipotolewa
nje ya uwanja kunako dakika ya 65 ya mchezo.
Dakika saba
baadaye Akombo Ukeyima akauweka mpira
wavuni na kuandika bao lingine na kuipa ushindi timu hiyo ya kutoka nchini Nigeria.
Matokeo ya michezo ya
kundi A
ASO Chlef 1-2 Sunshine Stars
Etoile du Sahel 0-2 Esperance
Katika kundi
B Zamalek inahitaji ushindi na mbeleko toka kwa klabu nyingine ya jijini Cairo,
Al Ahly angalau kupata nafasi ya kufika nusu fainali.
Ushindi kwa
timu hizo mbili za kutoka Misri ungewapa Ahly points 8 na kuongoza kundi B na
kuiweka Zamalek katika nafasi ya pili katika kundi.
Zamalek ambayo
haina point hii ilitarajiwa kuwepo dimbani dhidi ya TP Mazembe toka DRC mchezo ambao utapigwa bila ya
mashabiki huku milango ikiwa imefungwa kutoka na hali ya usalama kuwa ndogo
lakini pia mchezo mwingine wa kundi hilo Ahly yenyewe itakuwa ugenini nchini Ghana
kuwavaa Berekum Chelsea walio katika nafasi ya tatu katika kundi hilo.
Mazembe iliichapa
Zamalek kwa bao 2-0 nyumbani Congo wiki mbili zilizopita huku hongera nyingi zikipelekwa
kwa mlinda mlango Abdel Wahed Al Sayed na kuufanya mchezo huo kwenda dakika 70
bila bao.
Lakini naye Walid
Soliman akiisaidia Ahly kupata mvua ya mabao 4-1 dhidi ya Chelsea mjini Cairo.
Mabingwa
mara sita wa taji hilo barani Afrika Ahly wanaongoza wakiwa na points 9 wakati ambapo Mazembe na Chelsea wakitofautiana
kwa mabao ya kufunga na kufungwa wote wakiwa na points 4 nao Zamalek wakiwa
patupu kufuatia kufungwa katika michezo mitatu mfululizo.
Hata hivyo
endapo timu hizo za Misri zikipata ushindi katika michezo yao ya leo kule Cairo
na Accra huenda ikawapa nguvu Zamalek ya kuanza mbio za kusaka nafasi ya pili
kwa kuwa itakuwa nyuma ya Mazembe na Chelsea kwa point moja katika kundi ambalo
ndilo kundi la kifo.
Michezo ya kundi B
Berekum Chelsea v Al Ahly (Sunday, 1400
GMT)
Zamalek v TP Mazembe (Sunday, 2000 GMT)
Mshambuliaji
wa kimataifa wa Benin na Zamalek Razak Omotoyossi anaamini mabingwa hao mara
tano barani Afrika bado wako katika nafasi ya kuwania taji,lakini wanapaswa
kushinda michezo yao yote iliyosalia dhidi ya Mazembe, Chelsea na Ahly mjini Cairo.
No comments:
Post a Comment