Liverpool yaambiwa no kwa Butland
Meneja wa Birmingham
City Lee Clark ametangaza kuwa hana nia ya kumuuza mlinda mlango Jack Butland kwenda
Liverpool ama klabu nyingine yeyote.
Liverpool imekuwa
ikihusishwa kwa kuweka ada ya pauni milioni £7.5 kwa ajili ya mlinga mlango
huyo mwenye umri wa miaka 19 ambaye ni mlinda mlango kinda kuliko wote ambaye
aliidakia England katika mchezo dhidi ya Italy kule Berne jumatano.
Butland alikuwepo
katika kikosi cha England mwenye Euro 2012 pia alikuwa ni mlinda mlango namba
moja katika timu ya GB kwenye michuano ya Olympics 2012.
Mlinda mlango
huyo kwasasa ana kiwango cha kucheza katika timu yoyote katika ligi alianza
kuidakia Birmingham hapo jana baada ya
kuwepo kwa mkopo katika klabu ya Cheltenham inayocheza ligi ndogo maarufu kama ‘League
Two’ nchini Uingereza msimu uliopita.
Kwasasa ameanza
kupata umaarufu na kuanza kuvutia vilabu mbalimbali vya Premier League. Alionekana
mwiba katika mchezo ambao Birmingham ilikwenda sare ya bao 1-1 na Charlton katika
ligi ya Championship.
Everton seal Mirallas deal
Everton imetangaza
kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Belgium Kevin Mirallas toka Olympiakos ya
Ugiriki kwa mkataba wa miaka minne.
Mirallas
mwenye umri wa miaka 24 aliifungia timu yake mabao 20 kufuatia kushuka dimbani
katika michezo 25.
Everton
maarufu kama Toffees imeshinda mbio za kunasa sini ya Mirallas baada ya ada ya
pauni milioni £6 kukubaliwa na Olympiakos ijumaa jioni.
Mshambuliaji
huyo sambamba na ada hiyo kimsingi amekubali mambo yanayo husu maslahi yake
binafsi na marupurupu mengine na jana akafanyiwa vipimo vya afya ambavyo
alifanikiwa nah ii leo ametangazwa rasmi na klabu yake mpya.
Amenukuliwa Miralles
akisema
"nafurahi
kwa kuwa Everton ni klabu kubwa na binafsi hii ni fursa nzuri, nilijua Everton ilikuwa
ikinifuatilia kipindi kirefu na baada ya kuongea na meneja nikaamua kuja Everton.
"najua
hii ni klabu kubwa yenye mashabiki wengi na klabu yenye uwezo wa kushinda
michezo mingi katika Premier League. Ndio maana nimejiunga nayo."
Meneja David
Moyes amefurahia ujio wa mchezaji huyo na kusema ataipa nguvu kikosi chake
katika kampeni mpya hasa baada ya kuondokewa na Tim Cahill, James McFadden na
Joao Silva majira haya ya kiangazi.
Mirallas amekabidhiwa
jezi nambari 11 pale Goodison Park lakini hata hivyo kesho
hatakuwepo dimbani katika mchezo dhidi ya Manchester United.
Mshambuliaji
huyo anaweza kucheza nafasi nyingi za ushambuliaji ikiwemo winga wa pande zote.
Huko nyuma
amewahi kucheza vilabu kadhaa ikiwemo Standard Liege, St Etienne na Lille.
No comments:
Post a Comment