Kocha wa
kikosi cha pili cha simba kilicho fanikiwa kutwaa taji la BancABC Selemani
Matola amesema kwasasa ni jukumu la viongozi wa mpira nchini kuona ni namna
gani wataweza kuwasaidia vijana ambao wako wengi nchini na ambao wanaweza
kucheza soka endapo watapewa nafasi.
Matola
ambaye ni kiungo wa zamani wa Simba amesema hakuna haja ya kuendelea kugombea
wachezaji hasa wa kutoka nje ya nchi wakati wachezaji ni wengi hapa nchini
isipokuwa wanakosa kuendelezwa na
viongozi wa vilabu na shirikisho la soka hapa nchini tff.
Akiongea na
Rockersports Matola amesema watanzania wameona kuwa anaweza kufundisha soka na
ni faraja kwake kuongoza kikosi cha Simba ambacho kimetwaa taji la BancABC.
Ameongeza
kuwa soka duniani linachezwa na vijana na hivyo ni jukumu la wenye mpira
kuliona hilo na kulifanyia kazi.
Kikosi cha
pili cha Simba jumamosi kilitwaa taji la BancABC Sup8r 2012 chini ya kocha
Matola baada ya kuizamisha Mtibwa Sugar inayofundishwa na nahodha wa zamani wa
timu ya taifa ya Tanzania Mecky Mexime iliyokuwa imekamilika kila idara kwa
mabao 4-3.
No comments:
Post a Comment