Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam imeingi amktaba wa
mwaka mmoja na aliyekuwa kucha wa APR ya Rwanda Ernstus ‘Ernie’ Wilhelmus
Johannes Brandts ambaye ni raia wa uholanzi mkataba ambao umesaini hii leo
katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyoko katika makutano ya mitaa ya Twiga na
Jangwani Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Brandts anachukua nafasi ya Mbelgiji Thom Seintfiet
aliyetimuliwa kazi hivi karibuni kufuatia kutoleana maneno ya hovyo na
mwenyekiti wa klabu hiyo Yusufu Manji.
Mkataba huo wa mwaka mmoja umetiwa saini mbele ya
waandishi wa habari ambapo upande wa Yanga umewakilishwa na makamu mwenyekiti
Clement Sanga.
Akiongea mara baada ya zoezi la utiaji saini kukamilika Brandts amesema kimsingi amekubaliana na phylosophy ya klabu yake mpya ambayo amefafanua kuwa ni suala zima la nidhamu ndani na nje ya uwanja.
Amesema amejipanga kwa nguvu zake zote na kufanya kazi kwa moyo wake wote akizingatia mazungumzo yake aliyofanya na mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji ambaye alimueleza juu ya historia ya Klabu hiyo na Phylosophy ya klabu kwa ujumla.
Amesema kikubwa kwake ni kujenga uwezo binasfi zaidi wa kila mchezaji lakini pia jambo muhimu ni nidhamu na kama akisema mazoezi ni saa 12 asubuhi basi kila mchezaji anapaswa kutii hilo lakini pia atajitahidi kujenga mahusiano mazuri baina ya wachezaji wake.
kuhusiana na mchezo dhidi ya Simba amesema anajua ni mchezo wa ushindani lakini anaamini atakuwa na kikosi kizuri cha kiushindani zaidi na atafanya kila linalowezekana kupata ushindi dhidi ya Simba jumatano.
No comments:
Post a Comment