KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, September 29, 2012

LIGI KUU TANZANIA BARA SIMBA MARIDADI, AMIR MAFTAHA KUIKOSA MECHI YA YANGA.

Ligi kuu ya soka Tanzania Bara imeendelea tena hii leo ambapo mabingwa watetezi wa ligi hiyo Simba walikuwa wakiwakaribisha maafande wa jeshi la magereza Tanzania Prisons mchezo uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo Simba imefakiwa kuendeleza rekodi yake nzuri ya ushindi tangu kuanza kwa ligi hiyo baada ya hii leo kuwachapa maafande kwa mabao 2-1.
.
Prisons ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao lililowekwa nyavuni na mshambuliaji Elias Maguni kwa shuti ambalo lilimbabatiza mlinzi Juma Nyoso na kumpoteza mlinda mlango Juma Kaseja kabla ya mpira huo kutinga wavuni.

Mabao ya Simba yamepatikana kunako dakika ya 45 ya mchezo kupitia kwa Felix Sunzu aliyepokea posi ya Mrisho Ngasa.

Bao la pili limefungwa na Mrisho Ngasa kwa shuti ambalo lilimponyoka mlinda mlango wa Prisons na kutinga wavuni.

Katika hatua nyingi mlinzi wa pembeni wa Simba Amir Mftaha itabidi awe mtazamaji katika mchezo wa watani wa jadi Simba dhidi ya Yanga utakao chezwa jumatano kufuatia hii leo kupewa kadi nyekundu baada ya kumpiga bila mpira mchezaji mmoja wa Prisons ya Mbeya.

Mbali na Maftaha mchezaji mwingine atakaye kosekana katika mchezo huo ni Emmanuel Okwi ambaye alipewa kadi nyekundu katika mchezo wa Simba dhidi ya Ruvu Shooting.
 
Kwa matokeo ya mchezo wa leo, Simba imerejea kileleni katika msimamo wa ligi hiyo baada ya kufikisha jumla ya alama 12 na kufuatiwa na Azam fc yenye alama 10.

Ligi hiyo inaendelea tena kesho kwa mchezo mmoja ambao mabingwa wa kombe la Kagame Yanga watakapo teremka dimbani katika uwanja huo kwa kuwakaribisha Afrikan Lyon.

No comments:

Post a Comment