Mzee maarufu wa Yanga Yusufu Mzimba akiongea na Rockersports |
Mzee Mzimba akisisitiza kumuua mnyama jumatano |
Katika kuhakikisha mnyama anauwawa katika mchezo wa jumatano wa watani wa jadi katika soka la Tanzania Simba na Yanga mchezo ambao utafanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wazee wa Yanga pamoja na viongozi wa mikoa wa klabu hiyo wamekutana ili kuweka mikakati thabiti ya kupata ushindi mnono.
Akiongea na Rockersports katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyoko katika makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani mzee maarufu wa klabu hiyo Yusufu Mzimba amesema wameamua kufanya mkutano huo kwa lengo la kukusanya nguvu ya pamoja na viongozi wao wa juu wa Yanga ili kutoa msaada na uzoefu wao katika kufanikisha azma ya ushindi.
Amesema kinacho wasukuma zaidi ni kutokana na dhamira ya kweli ya ushindi kutoka kwa mwenyekiti wao Yusufu Manji akishirikiana na viongozi wengine wa kamati ya utendaji ambao kimsingi wameomba msaada kutoka kwao ili kufanikisha ushindi mnono utakao wafariji wana Yanga ambao bado wanaumizwa na kichapo cha mabao 5-0 cha mchezo uliopita.
Mzee Mzimba amesema yeye kama walivyo wanachama na wapenzi wengine wa Yanga bado wana kumbukumbu mbaya ya kichapo cha mabao 5 ambayo amesema yalitokana na uongozi uliomeguka wa Lyod Nchunga ambao ulikosa umoja na kupenyezwa hujuma za makusudi ili kuidhalilisha klabu yao.
Aidha amesema watajitahidi kwa kadri itakavyo wezekana wao kama wazee wa klabu kwa kushirikiana na uongozi wa klabu wakiongozwa na Manji, viongozi wa matawi na mikoa pamoja na kundi la vijana wa klabu hiyo kuhakikisha mnyama anauwawa jumatano hata kama si kwa idadi ya mabao 5 basi yasipungue mabao 3.
Jana katika makao makuu ya klabu hiyo kulifanyika mkutano maalum uliowakutanisha viongozi wa Yanga wa mikoa na wengine wa matawi makubwa ya jijini Dar es Salaam, klichoitishwa na mwenyekiti wa klabu hiyo Yusufu Manji kilicho kuwa na ajenda mbalimbali lakini kubwa ni juu ya mchezo wa Jumatano dhidi Simba mkutano ambao mpaka Rockersports inaondoka eneo la mkutano kilikuwa bado kikiendelea.
No comments:
Post a Comment