Mshambuliaji mwenye umri wa miaka 20 raia wa
Tanzania. Mshambuliaji huyu raia wa Tanzania amebatizwa jina na vyombo vya
habari vya nchini Misri la ‘Egyptian Slayer’ (YAANI MUUAJI WA WAMISRI), baada ya kufanikiwa kufunga goli katika kila
mchezo dhidi ya vilabu vikubwa vya nchini humo Al Ahly na Zamalek.
Mshambuliaji
huyo mpaka sasa amefanikiwa kutikisa nyavu mara sita katika michuano hii ya
vilabu bingwa barani Afrika ambapo mabao 4 ni dhidi ya vilabu vya Misri.
Mabao 3 kati
ya hayo akifunga kwa kichwa akionyesha ni namna gani alivyo hatari katika
kuruka hewani.
Abdel-Wahed El-Sayed - Zamalek (EGYPT)
Abdel-Wahed El-Sayed - Zamalek (EGYPT) mwenye umri wa miaka 35 ambaye pia ni
raia wa Misri ameonyesha kiwango cha kuvutia licha ya kwamba timu iliambulia
point moja kati ya points 15. Alikuwa ndiye pekee ambaye aliyevutia cha timu
yake.
‘Simba wa Afrika’, kama alivyo batizwa jina na
mashabiki wa Misri hususani wale wa timu yake ya alikuwa na kazi kubwa ya
kuhakikisha anatikisa nyavu za wapinzani hususani katika michezo ya ugenini.
Uwezo mkubwa
alionyesha katika mchezo dhidi ya TP Mazembe uliochezwa Lubumbashi alidhihirisha
wazi kuwa alikuwa ni hatari licha ya timu yake kupoteza kwa kufungwa mabao 2.
Sehemu ya
ulinzi ya Zamalek tatizo na kuruhusu mashambulizi lakini Abdel Wahed alikuwa
akipigana kusaka mabao.
Olorundare Dele - Sunshine Stars (NIGERIA)
Mshambuliaji huyu ana umri wa miaka 21 ambaye
pia ni raia wa Nigeria.
Olorundare
Dele mara zote amekuwa ni mshambuliaji hatari kwa wapinzani wa timu yake ya Sunshine
Stars katika hatua hii ya vilabu barani Afrika.
Mshambuliaji
huyu wakati mwingine amekuwa akitumika kama mshambuliaji wa pembeni na hiyo ndiyo
sababu ambayo imepelekea kikosi cha wanigeria kuwa kizuri katika mashindano.
Sunshine
Stars ambayo haina historia ya kuchukua taji lolote barani Afrika, ilifanikiwa
kufika katika hatua ya nusu fainali katika michuano hii ya kwanza ya vilabu
bingwa.
Akiwa ndiye
mchezaji wa mchezo yaani “man of the match” katika mchezo
dhidi ya ASO Chlef, Dele alifunga bao la kwanza na kutoa pasi ya mwisho
iliyozaa goli na hivyo kuwapa ushindi vijana hao maarufu kama Agugu
Boys na kupata points tatu muhimu.
Franck
Kom - Etoile du Sahel (TUNISIA)
Huyu ni kiungo raia wa Cameroon mwenye umri wa
miaka 20 ambaye alikuwa akifanya kazi kubwa katika hatua ya makundi katika
kikosi cha Etoile du Sahel.
Timu hii ya Tunisia
ilishindwa kufuzu baada ya michezo yake minne ya hatua ya makundi kutokana na
vurugu za mashabiki wake kuvamia uwanja katika mchezo dhidi ya wapinzani wao
wakubwa Esperance.
Kom alitegemewa
kuwa ni kiungo ambaye angeonyesha upinzani mkubwa katika sehemu ya kiungo baada
ya kuonyesha soka la kueleweka.
Soloman
Asante - Berekum Chelsea (GHANA)
Huyu ni mshambuliaji mwenye umri wa miaka 21 raia
wa Ghana.
Hivi karibuni
chama cha soka nchini Ghana kiliondoa mashaka juu ya uraia wa Solomon Asante
baada ya kutoa taarifa kuwa ni halali kuichezea timu ya Taifa ya Ghana ‘Black
Stars’.
Asante alitumika katika kikosi cha timu ya
taifa ya Bukina Faso miaka miwili iliyopita ukiwa ni mchezo wa kirafiki wakati
huo akiichezea ASFA Yennenga, ambapo pia aliibuka kuwa mfungaji bora wa ligi
kuu ya Bukina Faso ‘Burkinabé Premier League’ akiwa ana umri wa miaka 18.
Winga huyo
wa kulia alikuwa na uwezo mkubwa wa kuingian ndani na kutoa msaada kwa Emmanuel
Clottey, na kutengeneza nafasi za ushindi. Asnate alitajwa katika kikosi cha
timu ya Taifa ya Ghana kwa ajili ya michezo dhidi ya Malawi na Liberia.
Mohammed Abou-Treika - Al Ahly (EGYPT)
Akiwa na umri wa miaka 33 raia wa Misri licha
ya kwamba imesali mwezi mmoja kabla ya kutimiza miaka 34, Abou-Treika anaonekana
kupoteza uwezo wake wan soka wa ujana.
Kiungo huyu
wa chini ameonyesha bado ana uzoefu mkubwa katika michuano hii, amefunga jumla
ya magoli 6, Abou-Treika ndiye mfungaji
mwenye magoli mengi katika kikosi cha Al Ahly katika michuano hii.
Alifanikiwa
kufunga goli katika mchezo dhidi ya wapinzani wao wakubwa Zamalek na kuwaweka
katika nafasi nzuri katika msiammo wa kundi
Abou-Treika aliendelea
bado kuonekana gumzo licha ya kukosekana katika mchezo dhidi ya Berekum
Chelsea, baada ya kuwa na majukumu mengine katika michezo ya Olympic iliyofanyika nchini Engand.
Kwa bahati
mbaya kwasasa , Treika amesimamishwa kwa miezi miwili na klabu yake ya Al Ahly kutokana
na kugemea kucheza mchezo wa ‘Egypt Super Cup’ na huenda akakosekana katika
michezo ya kumalizia michuano ya ligi ya mabingwa Afrika.
Yannick
N’Djeng - Esperance Sportive de Tunis (TUNISIA)
Mshambuliaji huyu ana umri wa miaka 22 ambaye
ni raia wa Cameroon licha ya kwamba ana magoli 4 tu katika michuano hii lakini
bado ameonekana kuwa ni hatari katika michuano hii ya vilabu na ngumu kuzuilika
na mabeki.
N’Djeng mara
nyingi huwa anafunga magoli ya dakika za mwisho, alifunga goli la pili la Esperance
dhidi ya Sunshine Stars mchezo uliofanyika nchini Nigeria, lakini pia goli la
dakika ya 93 dhidi ya ASO Chlef wakati ubao ukisomeka 2-2, na mwishowe na
muhimu kuliko alifunga goli la pili dhidi ya Etoile du Sahel, bao ambalo
lilisababisha mashabiki kuvamia uwanja muda mfupi baada ya N’Djeng kushangilia.
Walid
Soliman - Al Ahly (EGYPT)
Huyu ni winga mwenye umri wa miaka 27 raia wa
Misri. Ni mjanja uwanjani na hii ni mara yake ya kwanza kucheza michezo hii ya
vilabu bingwa.
Alifunga magoli
mawili muhimu dhidi ya Berekum mchezo uliochezwa Cairo, katika mchezo dhidi ya Mazembe
alitoa pande la pasi muhimu kwa Emad Metab aliyekunga goli la uongozi la Ahly, lakini
pia kasi yake uwanjani katika mchezo dhidi ya Zamalek alikuwa mwiba kwa mlinzi
wa kulia Ahmed Samir.
Soliman alikuwa
ni mchezaji nyota wa mchezo dhidi ya Berekum Chelsea, wakati ambapo bosi wa
zamani wa Chelsea Hans van der Pluijm akitanabaisha kuwa Soliman ndiye mchezaji
wa mashindani na hutakiwi kukosa kumuangalia.
Tresor
Mabi Mputu - TP Mazembe (DR CONGO)
Huyu ni mshambuliaji raia wa Congo mwenye umri
wa miaka 26 mara nyingine anafanishwa kama Samuel Eto’o mpya hasa baada ya
kocha Claude le Roy kusema anaimani Mputu hana mlinzi wa kumzuia.
Mputu alikuwa
nahodha wa Mazembe katika michuano ya vilabu bingwa Afrika 2009 na 2010 pamoja
na kuonyesha kiwango safi katika fainali ya vilabu bingwa duniani.
Licha ya
kufanya majaribio mara mbili katika klabu kubwa ya nchini England Arsenal bado ,
Mputu ameendelea kusalia Lubumbashi, ambapo ameendelea kuwa nyota baada ya
adhabu ya kusimama miezi 12 kwa kuonyesha vitendo vya hovyo
Mputu amefunga
mabao 6 mpaka sasa ikiwa ni pamoja kufunga mara mbili katika mchezo dhidi ya Berekum
Chelsea, matokeo ambayo yameipeleka Mazembe katika nusu fainali.
Emmanuel
Clottey - Berekum Chelsea (GHANA)
Huyu ni mshambuliaji mwenye umri wa miaka 25 ambapo bila mashaka yoyote, Clottey anastahili
kuongoza orodha hii ya wakali.
Akiwa na umri
wa miaka 20 alikuwa ndiye mfungaji bora wa ligi ya Ghana ‘Glo Premier League’
akifunga jumla ya mabao 14.
Baada ya kuhangaika huku na huko barani Ulaya
ikiwa ni pamoja na kuelekea Austria na Denmark, kabla ya kurejea nchini Ghana, Clottey
amerejea Afrika Magharibi.
Clottey kwasasa
anaongoza kwa ufungaji katika ligi ya vilabu bingwa Afrika. Alifunga mabao
matatu pekee yake yaani ‘hat trick’ dhidi ya Zamalek, na goli moja dhidi ya Ahly
mjini Cairo, akaonyesha pia soka safi katika mchezo dhidi ya Mazembe mjini Lubumbashi.
No comments:
Post a Comment